Mtunzi: Enea Faidy
I lipoishia sehemu ya Saba ( kama hukuisoma BOFYA HAPA ) ..
....Mwalimu John alidhaniwa kufariki, hivyo harakati za mazishi ziliandaliwa.. Je John alikufa kweli?
Dorice alikuwa kwenye harakati za kutoroka, lakini kuna kitu kilimshtua..
Eddy alipewa sharti la kutofanya mapenzi na Doreen lakini tayari hamu ya mapenzi ilimvaa kwa kasi ya ajabu. Je atafanya mapenzi na Doreen?..
ENDELEA...
... MIPANGO YA MAZISHI kumzika mwalimu John ilikuwa tayari imekamilika, ndugu walikuwa tayari wamewasili kwa majonzi. Huzuni iliwatawala sana kwani mwalimu John alikuwa ndiye tegemezi la familia yote kwa ujumla. Kelele za vilio zilitawala mtaa mzima aliokuwa akiishi mwalimu John, kila MTU alisema lake juu ya msiba ule lakini ukweli haukujulikana.
Make wa mwalimu John alipoteza fahamu kila Mara huku akijutia tendon alilomfanyia mumewe kwa kumpiga na upawa kichwani .Lakini alijiahidi kutomwambia mtu yoyote akihofia kukamatwa kwa kosa la mauaji. Nyuso za watu wote zilitia huruma sana kwa kuondokewa na mwalimu John kipenzi cha watu wengi.
Walimu kutoka shule ya sekondari Mabango walikuwepo pale msibani wakimuaga mwalimu mwenzao.
Jeneza la gharama lilitengenezwa, mwili wa mwalimu John ukawekwa ndani ya jeneza. Make wa mwalimu John alikuwa haamini kama mume wake ndo anapelekwa kuzikwa.. Aliachia yowe Kali lililowashtua wote pale msibani "Rudi mume wangu.. Rudi mpenzi wangu usife..." Alilia mke wa John.
Wazazi wake walikuwa wakigalagala chini kama wehu,hawakujali vumbi lililokuwa limetapakaa ardhini kutokana jua Kali la kiangazi.
Hatimaye Jeneza lililokuwa limebeba mwili wa marehemu John likaingizwa kwenye gari kwaajili ya kupelekwa makaburini huku likisindikizwa na nyimbo za huzuni zinazopigwa misibani. Watu wote wakaelekea makaburini kwani magari ya kutosha yalikuwa yamekodiwa.
Mwalimu John alikuwa ndani ya Jeneza akilia kwa sauti ili Atolewe kwani alikuwa hajafa. Lakini hakuna MTU yeyote aliyesikia kilio cha Mwalimu John wala kuhisi, " Inamaana wananizika mzimamzima?" Alijiuliza mwalimu John huku moyo wake ukiwa umezimia kwa mile akionacho.
"Haiwezekani nizikwe mzima mzima! Hapana" alisema Mwalimu John huku akijaribu kujiinua lakini mwili wake ulikuwa bado mzito kama vile umegandishwa na barafu. Akiwa ndani ya jeneza hilo akasikia kicheko kikali sana kutoka kwa Doreen.
"Doreen nisamehe tafadhali" alijitetea Mwalimu John.
Machozi yalizidi kumtoka kwa kasi sana , ndipo alipokumbuka kosa lake kwa Doreen.
Zilikuwa ni wiki mbili tangu Doreen ahamie shule ya Mabango, kutokana na uzuri na utanashati wa mwalimu John. doreen alivutiwa nae sana hivyo akaamua kumwambia ukweli mwalimu wake kuwa anampenda na anahitaji kuwa naye kimapenzi. Mwalimu John alimtazama binti yule kwa jeuri na dharau kisha akamjibu " We mtoto ni mpumbavu sana! Umezunguka kote huko ukaona uniletee umalaya wako hapa? Mbwa koko wewe hebu niondokee hapa!"
"Mwalimu John hunitaki? Unanitusi? Sasa nitakuonyesha kazi!" Alisema Doreen kwa kujiamini sana kisha akaondoka zake
.
Wakati Mwalimu John akiendelea na kumbukumbu hizo ghafla akahisi jeneza lake linanyanyuliwa Tayari kwa kumuweka kaburini... *********
Dorice alipokuwa akitembea ghafla akazungukwa na chatu mkubwa sana kila upande. Dorice alishtuka sana, mapigo yake ya moyo yakamwenda kasi sana akiwa haelewi la kufanya.
Kutokana na woga Dorice aliangusha chini mkoba aliokuwa ameubeba lakini ghafla akakumbuka kitu. Akaokota mkoba wake kwa ujasiri sana kama vile hakumjali chatu yule kisha akatamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe. Ghafla bin vuu chatu yule akatoweka kimuujiza, Dorice akaendelea na safari yake.
Alitembea mwendo wa kama dakika tano hatimaye akafanikiwa kuiacha mipaka ya shule, akaingia barabara kuu ya kokoto ambayo ilizingirwa na miti kila upande. Akaendelea kupiga hatua moja baada ya nyingine kuelekea alikokusudia.
Safari ilikuwa ndefu sana na Giza likazidi kuiteka dunia ingawa mbalamwezi ikawa taa kwa msichana yule mwenye kujiamini.
Dorice alitembea taratibu baada ya kuchoka kutokana na mwendo mrefu hatimaye akafika kwenye kijito kidogo kilichotawaliwa na ukimya wa ajabu. Hakukiwa na sauti ya vyura wala wadudu palikuwa kimya mno. Dorice akavuta pumzi ndefu na kuishusha taratibu sana kisha akaketi pembeni ya kijito kile kimya.
Alikaa karibia robo SAA nzima akiwa ameinamisha kichwa chake ghafla akasikia kishindo kizito ambacho kilimshtua mawazoni.
*********
Eddy aliendelea kumng'ang'aniza Doreen wafanye mapenzi lakini Doreen aliendelea na msimamo wake ule ule kuwa hawezi kufanya mapenzi.
"Doreen tafadhali mpenzi...!"
"Siwezi Eddy!"
"Hapana Doreen, kama ni hivyo niruhusu niwe na msichana mwingine!"
"Kwa hilo usije kuthubutu maana utahatarisha uhai wako?"
" kivipi?"
"Elewa hivo"
Eddy alishtuka kidogo lakini akaachana na mawazo hayo akaendelea kumbembeleza Doreen. Doreen aliendelea kukataa Katakata ingawa nayeye pia alitamani kufanya mapenzi na Eddy ila kuna kitu alikumbuka kikamtia hofu, akazidi kumkatalia.
Uvumilivu ulimshinda kabisa Eddy akajikuta anamtoa Sketi Doreen huku nae akishusha suruali yake. Akambwaga chini Doreen na kutaka kufanya nae mapenzi, kabla hajafanya chochote Eddy aliachia yowe Kali sana....
ITAENDELEA.