RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU TISA

Riwaya:Mwanafunzi Mchawi (A Wizard Student) - Sehemu ya Tisa
Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia Sehemu ya 8 ( BOFYA HAPA  Kama Hukuisoma )
..Mwalimu John alipelekwa makuburini kwaajili ya mazishi ingawa yeye alijiona yuko hai. Dorice alikuwa njiani baada ya kutoroka shulen, na alipofika kwenye kijito kidogo alishtushwa na kishindo kikali.
Eddy alifikia hatua ya Mwisho kutaka kufanya mapenzi na Doreen lakini kabla ya kufanya hivyo aliachia yowe Kali.
SONGA NAYO UJUE KILICHOJIRI....
....VIJANA wanne wenye nguvu walinyanyua jeneza alililokuwamo Mwalimu John kisha taratibu walipiga hatua kuelekea kwenye nyumba yenye pembe NNE na kina kirefu kiasi aliyotengenezewa mwalimu John.
Sauti za vilio zilizidi kutia simanzi katika eneo lile LA makaburini. Nyimbo za huzuni zilitawala eneo hill huku kila mmoja akisikitika moyoni mwake.
Ndani ya jeneza hilo mwalimu John alikuwa akihangaika sana kuwaita vijana wale ili wasimzike lakini katu hakusikika. Alizidi kupiga kelele za kuomba msaada lakini ikabaki kuwa kazi bure. Sauti iliyojaa huzuni kuu ya mkewe Monalisa ilizidi kupenya vyema masikioni mwake, hali hii ilzidi kumtia simanzi mwalimu huyo ambaye sasa alikuwa amekata tamaa ya kuishi tena.
"Daah Doreen hafai" alijisemea mwalimu John huku machozi yakimtiririka kwa kasi kwani bado alikuwa haamini kama kweli anazikwa akiwa mzima.Vijana wale walilishusha jeneza like lenye mapambo ya kupendeza ndani ya kaburi kisha wakatulia kidogo ili mchungaji atupie neno LA mwisho.
Mchungaji alichukua udongo kidogo na kusogelea vyema kwenye shimo alilowekwa mwalimu John."Uliumbwa kwa mavumbi hakika utarudi mavumbini, Bwana alitoa Bwana ametwaa jina LA Bwana lihimidiwe... " Mchungaji aliyasema maneno hayo kwa huzuni kisha akaumwaga kaburini udongo ule aliokuwa ameushika mkononi.
Mwalimu John aliyasikia vyema maneno hayo yaliyouchoma moyo wake kama mkuki wenye sumu. Hakika mwalimu John alikiri kuwa kweli duniani kuna watu na viatu, Doreen alikuwa kiatu chakavu kisichofaa kuvaliwa hata na kichaa.
Vijana walishika vyema sepetu zao ili waanze kutupa udongo kaburini na kumzika mwalimu John lakini kabla hawajaanza kutupa udongo, kilizuka kimbunga kikali cha ghafla kilichofanya watu wapoteane. Jeneza likafunuka ghafla mwalimu John akainuka kutoka kwenye jeneza.
********
Eddy aliachia yowe Kali sana ambalo lilijirudia Mara kadhaa. Yowe hill lilitokana na maumivu makali sana aliyoyapata kwenye sehemu zake za siri. Maumivu yalikuwa makali sana hivyo alianguka chini na kupoteza fahamu.
Wakati wote huo Doreen alikuwa amebadilika sura na kuwa sura kama sura ya paka. Kucha zilimtoka kama za chui anayekabiliana na hatari. Kichwa chake kilikuwa na mapembe marefu. Hivyo akawa na umbile la kutisha sana ambalo hakuna kiumbe wa kawaida angeweza kustahimili kumtazama hata kwa nusu sekunde.
Licha ya kwamba Doreen alikuwa kwenye umbile lile la kutisha lakini alionekana mnyonge sana. Machozi ya damu yalikuwa yakimshuka taratibu kwenye macho yake. Alimsogelea Eddy na kukaa karibu yake huku akimgusa taratibu mwilini mwake.
"Eddy mpenzi wangu nakupenda sana.. Nisamehe kwa kilichotokea.. Halikuwa kusudio langu hata kidogo, ila umelazimisha... Nakupenda sana na ninakuahidi kukupenda maisha yangu yote...!" Alisikika Doreen akiongea kwa huzuni ila sauti yake ilikuwa ilikuwa nzito ya kutisha iliyoambatana na mwangwi mkali. Doreen alizidi kulia kwa huzuni sana na taratibu sura yake ilianza kujirudi. Akawa Doreen yule aliyezoeleka.
Machozi yakawa hayamkauki kwa kitendo alichomfanyia Eddy mwanaume ampendaye sana.Doreen akampandisha Eddy suruali kisha akatulia kimya akimsubiri azinduke.
Lilipita SAA zima ndipo Eddy akapiga chafya ya kwanza.. Doreen alimtazama Eddy kwa huzuni na huruma nyingi lakini Eddy hakufumbua macho. Baada ya robo SAA Eddy akapiga chafya mbili mfululizo kisha akayafumbua macho taratibu lakini hakuweza kuona chochote kutokana na Giza Nene lililozingira kila upande, Eddy akaogopa akataka kukimbia lakini mwili wake ulikuwa mchovu sana kama MTU aliyefanya kazi ngumu kupita kiasi. Akajishangaa sana .
"Eddy mpenzi. ." sauti ya Doreen ilimshtua Eddy na kumfanya ajue kuwa hayupo peke yake. Eddy akageuka na kumwona Doreen kwa mbali kwani Giza lilimzuia asionekane sana .Kumbukumbu zikamrudia Eddy kichwani akaikumbuka ile sura ya kutisha ya Doreen aliyomwona nayo kabla ya kupoteza fahamu.
"Toka! Usiniguse! Ushindweee.. !" Aliropoka Eddy huku akikikimbia bila kuelewa nguvu zimetoka wapi .
"Eddy!" Aliita Doreen lakini Eddy alikuwa tayari amekimbia.
"Oh! Shiit!" Alisema Doreen bila kuelewa la kufanya.Akasimama kwa muda kisha akaamua kuondoka zake eneo lile.
Eddy alifika bwenini kwao akakuta mlango umefungwa kwani wenzake walikuwa darasani kwa vipindi vya usiku(prep. Time). Eddy alisonya kwa hasira akiwa ameuegamia mlango huku kashika kufuli.
Ghafla wazo likamjia aliamua kwenda mlango wa dharula na kuingia bwenini. Woga ulimjaa ila hakuweza kwenda darasani aliamua kulala na kujifunika blanketi gubigubi.Usingizi ukampitia mpaka asubuhi.
"Eddy vipi mbona umelala sana, Jana ulikula mzigo kwa kasi nini?"
Alitania Jackson rafiki kipenzi wa Eddy baada ya kumwamsha.
"Vipi kumekucha" alisema Eddy kwa sauti ya nyono.
" hahah Eddy Yale mambo hayataki papara, hebu amka bhana! "
Jackson alicheka kisha akamfunua blanket Eddy.Eddy alijivutavuta kisha akaamka na kwenda bafuni kuoga .Alipofika bafuni aliwakuta wanafunzi wenzake wengi wakioga. Bila wasiwasi wowote Eddy alivua nguo zake na kuanza kuoga. Ghafla wanafunzi wenzake wakabaki kumshangaa Eddy, wakaanza kukonyezana kisha wote wakaanza kumtazama Eddy kwa wizi.
Eddy hakujua lolote akaendelea kuoga kwa kujiachia sana.
Wanafunzi hao wambeya hawakukomea hapo Bali walitoka nje na kuwaita wenzao ambao pia wakaingia bafuni mle wakijifanya kunawa nyuso zao kumbe walizuga tu, lengo kuu ilikuwa kumtazama Eddy.
*********
Dorice alishtushwa na kishindo kile pale mtoni. Akageuka kutazama nyuma , hakuamini macho yake kwani alimwona MTU mrefu sana akiwa amesimama nyuma yake. Dorice aliogopa sana akatetemeka.
"Unafanya mini hapa?" Like jitu refu lilimuuliza Dorice kwa ukali.
"Napumzika.. Nim..nimechoka" Dorice alijibu kwa kutetemeka.
"Umetokawapi na unaenda wapi?"
"Nimetoka Mabango.. Naenda mjini..!"
"Hahahahah kwanini ukae hapa? Hii ardhi yetu.. Na muda huu ni sherehe yetu umetusumbua... Hivyo utakuwa kitoweo chetu.." Lilisema jitu lile. Dorice alitetemeka kupita kiasi, jitu lile likamsogelea Na kumshika mkono kisha wakatoweka.....
ITAENDELEA.....

Related Post

Previous
Next Post »