RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 40
RIWAYA:MWANAFUNZI MCHAWI
MTUNZI:ENEA FAIDY
Sehemu ya 40
....Eddy alisimama kwa muda huku akiyashangaa yote yanayoendelea. Alishindwa kuamini kama kinachoendelea pale kilikuwa na ukweli ndani yake. Alifuta macho yake na kutazama tena, safari hii macho yake yalitua moja kwa moja kwa Doreen aliyekuwa amepiga magoti mbele yake huku akilia kwa uchungu na majuto mengi.
"Nisamehe Eddy kwq kukufanyia ukatili huu. Nimekutesa sana wewe na familia yako... Nisamehe tafadhali" alisema Doreen huku akilia kwa uchungu hali iliyodhihirisha majuto aliyokuwa nayo moyoni mwake. Hata hivyo Eddy hakuweza kuzungumza chochote zaidi ya kumtazama Doreen kwa hasira huku machozi yakimtiririka machoni mwake. Aliumanisha meno yake kwa hasira huku akitamani kuiondoa roho ya Doreen kwani mateso aliyompa maishani mwake ilikuwa ni vigumu kusahaulika. Mateso aliyokuwa nayo yalijaa fedheha na aibu isiyositirika. Machozi yalimshuka taratibu machoni mwake huku akimtazama Doreen.
"Naomba unisamehe Eddy ili adhabu ninayopata ipungue walau kidogo... Nateseka Eddy" Doreen alizidi kumsihi Eddy lakini maneno yake ilikuwa ni kama kujilisha upepo kwani Eddy hakuukubali msamaha wake.
Wanawake waliokuwepo eneo lile walijisikia aibu kwa kuona wanawake wenzao wapo uchi wa mnyama. Wakatoa khanga zao na kuwapa akina Doreen wazivae lakini hata hivyo ilikuwa vigumu kwa akina Doreen kupokea khanga zile kwani maumivu yalikuwa Makali mno kwenye miili yao. Kila Mara walihisi moto ukiwawakia katika ngozi zao. Ikawabidi wanawake wale wawafunike kwa lazima ili kuwasitiri.
Ghafla mwili wa Maimuna ukaanza kubadilika na kuwa mweusi kama mkaa. Akajiviringa viringa kama nyoka pale sakafuni huku akitoa mlio kama wa mbuzi kisha akatoweka mbele ya macho ya watu. Wote waliogopa sana, baadhi ya watu walijikaza kisabuni na kuendelea kubaki pale huku wengine wakikimbia sana na kuondoka eneo lile.
Doreen alibaki pale huku akiendelea kumsihi Eddy amsamehe. Lakini Eddy alikuwa na moyo mgumu sana wa kumsamehe kiumbe yule.
"Hustahili kuishi Doreen... Kufa tu.." Alisikika Eddy kwa sauti iliyojaa hasira.
"Kweli! Afe tu huyu! Tumuue!" Walisikika Raia waliokuwepo eneo lile.
"Nitakufa ndio ila naomba unisamehe.. Najua nimekukosea sana... Sitaki nife kabla hujanisamehe!" Alisema Doreen.
"Kwa mateso uliyonipa siwezi kukusamehe... Umenitesa sana... Sijui nani amekuadabisha namna hii na kukudhalilisha hivi... Amenifurahisha sana" alisema Eddy kwani hakujua lolote linaloendelea kuwa Dorice ndiye aliyefanya yote hayo.
"Na kwa jinsi ulivyonifanyia.. Daima siwezi kumwamini mwanamke! Naapa!" Alisema Eddy lakini kuna sauti ilimnong'oneza masikioni mwake
"Usiseme hivyo... Niamini Mimi" Eddy alishtuka sana akaangaza macho huku na kule pasipo kuona mtu aliyemnong'oneza. Sauti ile haikuwa ngeni sana masikioni mwake ila alishindwa kujua ilikuwa ya nani. Akatafakari kwa muda kisha akaipotezea sauti ile na kuendelea kumtazama Doreen.
"Eddy hutaki kunisamehe?" Aliuliza Doreen kwa sauti ya upole. Eddy akatafakari kidogo, akagundua kutomsamehe binadamu mwenzake ni kosa kubwa kwani yeye hutenda dhambi nyingi lakini husamehewa na Mungu.
"Nimekusamehe.. Ila sitokusahau!"
"Asante..."
Wakati akizungumza hivyo ghafla haja ndogo ilimbana sana Eddy, hakuielewa hali ile kwani tangu sehemu zake za siri ziondolewe hakuwahi kubanwa na haja ndogo hata Mara moja. Eddy alijishangaa sana akaamua kukimbia na kwenda msalani ili kuona kama angeweza kutoa taka mwili inayojulijana kama mkojo.
Alipofika chooni alishusha kidogo suruali yake na bila kutarajia akakuta sehemu zake zimerudi. Eddy hakuamini macho yake, akataka kujihakikishia kama kweli zitafanya kazi. Akakojoa na kweli jaribio lake likazaa matunda kwani alifanikiwa kukojoa kwa Mara ya kwanza.
"Mungu wangu! Mbona siamini!" Alisema Eddy kwa mshangao na furaha ya ajabu. Akajikuta anaruka ruka kule chooni shangwe kuu. Ghafla akahisi kuna mtu nyuma yake, Eddy akageuka haraka na bila kutarajia akakutana na uso uliojaa tabasamu wa Dorice.
"Eddy mpenzi nakupenda sana.. Nimefanya yote Haya kwaajili yako... Ili uone thamani ya upendo wangu.. Narudia tena niamini Mimi! Nakupenda!" Alisema Dorice. Eddy alibaki kimya akiwa ametoa macho kwa mshangao.
"Wewe ni jini"
"Hapana!"
"Sasa umefikaje hapa"
"Sina nia mbaya.. Nilitaka tu nikusaidie kwa tatizo lako... " alisema Dorice.
"Asante sana... Nashukuru Dorice... " alisema Eddy na kumkumbatia Dorice bila woga.
"Unanipenda?"aliuliza Dorice.
"Nakupenda sana!" Alisema Eddy kisha wakakutanisha midomo yao na kupeana mabusu. Licha ya kwamba Dorice alifahamu fika kuwa kufanya vile lilikuwa kosa kubwa sana kwa Mansoor lakini hakujali hilo kwani upendo wake wote ulikuwa kwa Eddy, alimpenda kupita kiasi.
"Wewe ndo mwanaume wa maisha yangu Eddy... Tangu nimekutana nawewe siku ya kwanza na ukanambia unanipenda sikutamani uniache hata kwa sekunde moja" alisema Dorice kwa sauti iliyojaa huba.
"Nakupenda pia Dorice... Wewe ni mwanamke pekee uliye kwenye ndoto zangu" alisema Eddy.
"Asante Eddy nitakuja wakati mwingine" alisema Dorice na kupotea.
"Doriiiiiice! Usiache kuja" alisema Eddy kwa sauti lakini Dorice alikuwa ameshaondoka.
Eddy alitoka nje akiwa na furaha sana. Alitamani hata kumwonesha kila mtu sehemu zake za siri ili ajue kuwa anazo.
Alipofika pale nje alikuta Doreen anavuja damu sana kwani wananchi walishaanza kumtupia mawe. Polisi walikuwa wamefika tayari eneo lile na kumchukua Doreen ili asiumizwe zaidi. Kwa mbali alionekana Dorice akimtazama Doreen na kumwambia kuwa yeye ndiye aliyefanya yote Yale. Lakini alipokuwa akizungumza hakuna aliyemwona zaidi ya Doreen na Eddy.
Doreen alichukuliwa na gari ya polisi na kupelekwa hospitali ili akatibiwe majeraha yake.
Lakini hata hivyo watu wengi walifika mpaka hospitali ingawa hawakuruhusiwa kuingia.
Doreen alianza kusaidiwa na madaktari , na baada ya kufungwa majeraha yake aliwaomba kitu madaktari.
"Kabla sijafa naomba mniitie mchungaji pamoja na waandishi wa habari" alisema Doreen kwa sauti ndogo iliyosikika kwa shida.
"Bado haupo vizuri... Unatakiwa kupumzika..." Alisema daktari mmoja.
"Tafadhali dokta nitajitahidi tu... Lakini cha kwanza nataka nikutane na hawa watu kabla sijafa..." Alisisitiza Doreen.
"Unataka kuwambia nini?"
"Kwanza nataka nitubu.. Pili Nataka niwaambie watu siri nzito kuhusu maisha yangu" alisema Doreen na kuwafanya madaktari wale washawishike na kufanya kama walivyoambiwa.
Alitwa mchungaji wa kanisa Fulani kisha wakaitwa waandishi wa habari wa vituo vya televisheni pamoja na radio ili warekodi kile alichotaka kuzungumza Doreen. Wote walikuwa na hamu ya kusikia kile wanachotaka kuambiwa na Doreen.
Na wakati huohuo taarifa za kilichomtokea Doreen zilikuwa tayari zimesambaa nchi nzima kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
MWISHO.
KAA TAYARI KWA MSIMU WA PILI WA RIWAYA HII UTAKAO KUJIA HIVI KARIBUNI. UTAPATA KUJUA MENGI YALIYOKUWA YAMEJIFICHA NYUMA YA PAZIA, UTABURUDIKA NA KUELIMIKA PIA.
JE UMEPATA FUNZO GANI??
RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU 38 NA 39
RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 38 & 39
MTUNZI:Enea Faidy
.....Mr Aloyce bado hakumuelewa vizuri mkewe kwa kauli aliyoisema. Kauli ile iliibua utata mkubwa kichwani mwake na kumtaka mkewe amueleze ukweli.
"Niambie mke wangu... Nini kinaendelea? Maana Mimi sielewi!" Alisema Mr Aloyce kwa sauti ya upole ili mkewe amweleze ukweli wote. Lakini kwa bahati mbaya sana Maimuna alisita kueleza ukweli ambao alitaka kumwambia Mr Aloyce.
Viboko mfululizo vilivyosikika kwa sauti kubwa vilimshukia Maimuna na kumfanya ahangaike kupita kupita kiasi. Aligalagala pale chini kama nyoka aliyepondwapondwa kichwa chake. Sauti na yowe la kilio viliibuka kwa Maimuna kwani alishindwa kuvumilia maumivi ya viboko alivyochapwa na MTU asimfahamu.
"Nasemaaa!nasemaaa!" Alisema Maimuna huku akilia.
Mr Aloyce na Mlinzi wake walibaki na mshangao kwani kila walichokiona walihisi ni muujiza tu. Walibaki kimya huku wakimshangaa mwanamke yule.
"Aloyce... Mimi ni mchawiiii.." Alisikika Maimuna na kwa bahati mbaya sana alishindwa kuongea kwa sauti ndogo hivyo sauti ilipaa sana na kuwafanya wapita njia na majirani kujazana sana nje ya geti kwa Mr Aloyce. Kwa uzito wa adhabu alioipata Maimuna ilimbidi tu aseme ukweli wote uliomwacha mdomo wazi Mr Aloyce.
"Naitwa Maimuna.. Sio mama yake Eddy kama ulivyodhani..." Alisema Maimuna na kumfanya Aloyce ahamaki. Alichanganyikiwa sana na kushindwa kuzungumza.
"Nisamehe Aloyce... Nilikuja kuiteketeza familia yako.... Mkeo alishaliwa nyama ... Mimi nilikuja kumlinda Eddy ili sehemu zake za siri zibaki mikononi mwa Doreen"
"What? Ati nini? Kwanza Doreen ni nani?" Mr Aloyce alijikuta anauliza maswali matatu mfululizo huku hasira zikiwa zimempanda kupita kiasi. Alitamani achukue jiwe zito na kumponda nalo mwanamke yule.
"Ni mchawi... Alikuwa anasoma na Eddy..." Alisema Maimuna huku akilia kwa sauti kubwa.
"Oh! Shit!" Alisikika baba Eddy.
Watu waliokuwa pale nje walizidi kutafuta upenyo wa kuingia mle ndani. Lakini geti lilikuwa limefungwa, kelele nyingi kutoka nje zilizidi kusikika.
"Mchawiiiiii! Mchawiii! Tufungulie tumwadhibu huyo mchawiiii!! Funguaa! Mwanamke mchawi hafai kuishi!!" Sauti zile kutoka nje zilimhamasisha mlinzi kufungua geti na kuwaruhusu watu waingie. Cha ajabu watu wale waliingia wakiwa wameshikilia silaha za aina mbalimbali. Wengine mawe wengine visu huku wengine wakiwa wameshikilia fimbo na mapanga. Hali ilichafuka sana pale ndani.
Umati wa watu ulikuwa uvamia uwanja wa Mr Aloyce tayari kwa kumwadhibu mchawi aliyesababisha kilio na majonzi katika familia ya ile iliyokuwa imejaa upendo na amani hapo awali."Tuue tu... Afe Huyo" walisema. Ghafla Maimuna akabadilika na kuwa kiumbe tofauti na vile anavyofahamika wote wakashtuka.
*****
Doreen aliendelea kushangaa kwa hofu sana ndani ya chumba kile. Upepo mkali uliovuma chumbani mle na kuangusha baadhi ya vitu vilivyokuwa vimewekwa vizuri ulimfanya Doreen ajione mdogo kama sisimizi juu ya janga lile.
Akiwa bado haelewi la kufanya ghafla sura ya MTU aliyemfahamu ikatokea mbele yake na kumfanya Doreen apigwe na mshangao wa hali ya juu.
"Haa! Dorice!" Alisikika Doreen akiita kwa mshangao.
"Mimi hapa! Sema nikusikie!" Alisema Dorice kwa sauti iliyojaa dharau kupita kiasi. Kisha kabla hajaendelea na lolote akanyoosha kidole chake ukutani na ghafla kikatokea kama runinga pana iliyoonesha siku ambayo Doreen alimpaka kamasi usoni kiuchawi ili asipendwe na Eddy. Kisha akaonekana Doreen akimkata Eddy sehemu zake za siri.
"Ulikuwa mjanja sana sio?" Alisema Dorice. Doreen hakuamini macho yake alitetemeka kwa hofu kupita maelezo.
"Do..Dor...Dorice... Umepata wapi huo ujasiri wa kunitisha kiasi hicho?" Aliongea Doreen kwa kigugumizi sana. Dorice alimtazama Doreen na kucheka kidogo huku akitembeatembea ndani ya chumba kile.
"Ulininyang'anya penzi langu kinguvu kwa mtu nimpendae sana.. Cha ajabu ulitaka kumharibia yeye na familia yake... Kwanini wewe in katili na mbaya kitabia kuliko sura yako?" Aliuliza Dorice.
"Tafa..Tafadhali Dorice nisamehe.."
"Nimekusamehe tangu zamani... Ila nataka kukufunza adabu. Umeua wengi sana wasiokuwa na hatia umewaharibu wengi sana bila kosa." Alisema Dorice na kutoweka machoni mwa Doreen.
Doreen alichanganyikiwa mno, lakini kilia alipotaka kupotea na kumtoroka Dorice hakuwa na nguvu, kwani Dorice alikuwa na nguvu nyingi mno ambazo zilimsaidia kufanya kila alichokitaka. Na hakuna mchawi ambaye angeweza kumshinda Dorice kwa wakati ule.
Ghafla bin vuu! Kichapo kikali kikamshukia Doreen. Alihisi mawe mazito yanamshukia kichwani mwake na kumpiga kwa nguvu. Alihisi maumivu makali mno. Akapiga ukunga mkali baada ya kushindwa kuvumilia maumivu Yale. Hakuona sababu ya yeye kuendelea kukaa ndani ya chumba kile huku akitaabika akaamua kufungua mlango na kutoka nje ya chumba huku akilia kwa sauti kali . kilio chake kiliwashtua wengi na kuwafanya watoke njee kutazama kulikoni.
Umati wa watu ulifurika kumtazama Doreen pale nje. Alikuwa uchi wa mnyama huku akipiga kelele sana.
"Naacha uchawiii... Mimi si mchawi...uwiiiii... Nisaidieni" alilalama huku akipiga mbio bila kujali kuwa hajavaa nguo yoyote.
Watu walianza kumfuata huku wakipiga kelele "mchawii! Mchawiiii" "masikini we! Binti mzuri hivi kumbe ana mambo ya uchawi?" Walisikika watu wakiongea vikundi vikundi.
Watu walikazana kupiga picha huku wengine wakiokotw mawe na kumfukuza Doreen huku wakimtupia mawe.
Doreen alikimbia sana huku akipiga kelele sana.
Ghafla mama mmoja alipiga kelele sana
"Huyu mtoto aliinibia pesa zangu mgahawani kumbe ni mchawi! Alaaniwe!"
"Mimi alikuja dukani kwangu akataka aniwangie Leo ameumbuka" walizungumza yule mama wa mgahawa ambaye alitapeliwa na Doreen kwa mazingira ya kutatanisha sana ndipo alipojibiwa na mwanaume mwingine ambaye Doreen alijaribu kumuwangia ili aibe pesa.
Doreen alizidi kupiga mbio sana huku umati ule wa watu mjini Iringa ukizidi kumfata kwa kasi wakiwa wameshika mawe na wengine viboko.
*****
Baba Pamela alikuwa ametulia kidogo huku akimtazama binti yake kwa masikitiko makubwa.
"Daddy najisikia hasira hata kumtazama mama" alisema Pamela huku akilia.
"Hutakiwi kuwa hivyo... Nataka tufanye jambo hapa!"
"Jambo gani mume wangu?" Aliuliza mama Pamela.
"Nataka tumwombe Mungu mpaka atujibu juu ya binti yetu"
"Hakuna tatizo mume wangu.." Alisema mama Pamela kwani tayari maneno ya mumewe yalimpa nguvu hata ya kuzungumza.
"Pamela una amini kama Mungu anaweza kutenda mambo ambayo sisi hatuwezi?"
"Ndio naamini... Lakini..."alisema pamela
"Lakini nini? Ukiwa na imani hutakiwi kutilia shaka.."
"Sawa baba niombee tu.."
Baba Pamela aliwataka wote wapige magoti kisha wakaanza na nyimbo na baada ya hapo akaanza kufanya maombi. Aliomba sana akiwa anataka Mungu amrudushie mwanae titi lake.
Radi Kali zikaanza kupiga katika nyumba zilipiga radi nyingi wakati baba Pamela akiendelea kusali kwa bidii na imani sana. Ghafla akawaambia watoke nje wote.
"Roho wa Mungu ananiambia kuna kitu kimefukiwa pale nje ili kutuangamiza" alisema baba Pamela kisha wote wakatoka nje. Baba Pamela aliongoza njia mpaka Pale ambapo Mama Pamela alifukia sahani iliyokuwa na kinyesi. Wakafukua.
Cha ajabu akatokea nyoka mkubwa sana ambaye hakuna aliyetarijia kama angekuwa pale.
"Mungu wangu!" Alisikika Mama Pamela akizungumza kwa woga. Baba Pamela alizidi kumwomba Mungu mpaka yule nyoka alipobadilika na kuwa na sura ya Doreen lakini mkiani akabaki kuwa nyoka. Wote walistaajabu sana huku wakitetemeka kwa woga...
RIWAYA:MWANAFUNZI MCHAWI - SEHEMU YA 39
...."Ina maana Doreen ni mchawi kiasi hiki?" Alijikuta anaropoka kwa mshangao mama Pamela. Pamela alizidi kushangaa huku akimtazama mama yake kwa mshangao kisha akimtazama chatu yule mwenye sura ya Doreen. Baba Pamela aliendelea na maombezi yake kwa imani kali. Yule chatu alijigeuza geuza kwa vitisho vikali sana huku akijaribu kupambana Na Baba Pamela kwa kujitoa kwenye lile shimo dogo.
Lakini kwa bahati njema chatu yule alipigwa na radi Kali sana iliyoharibu uso wake na kuweka mipasukopasuko iliyoacha damu ichuruzike kirahisi. Baba Pamela hakuacha kuomba na kuithibitisha imani yake thabiti. Ghafla ukatoka moshi mkali kutoka kwenye mdomo wa sura ya Doreen iliyopo kwa yule chatu.
Moshi ule ulikuwa wa ajabu sana Kwani ulikuwa katika mstari ulionyooka mpaka kifuani kwa Pamela, na hata Pamela alipojaribu kukimbia moshi ule ulimfuata kila alipoenda na kumfanya Pamela aogope zaidi. Pamela alipoona hawezi kuukwepa moshi ule akasimama wima akisubiri kuona kitakachotokea huku akihema nguvu sana.
Moshi ule ulitua taratibu kifuani kwa Pamela kisha ule mstari uliokuwa umejitengeneza ukapotelea kifuani kwa Pamela taratibu sana. Pamela alijishangaa sana Kwani alihisi mabadiliko Fulani mwilini mwake. Alitulia kimya huku akimtazama baba yake.
Baba Pamela alipohitimisha maombi yake yule chatu alipigwa radi Kali kisha akatoweka machoni kwa wanafamilia wale.
"Jina la Bwana lihimidiwe kwani ametenda tulichokitaka.. Amejidhihirisha mbele yetu.. Oh asante Bwana wa Majeshi" alisikika baba Pamela huku akiinua macho yake na mikono yake juu ili kumshukuru Mungu kwa ajili ya maombi yake.
"Pamela hebu jitazame kifuani kwako" alisema Baba Pamela huku akitabasamu na kutoa kitambaa laini mfukoni na kujifuta jasho lililokuwa limetapakaa usoni kwake kama chemchem ya maji.
Mama Pamela alimsogelea mwanae na kumsaidia kushuhudia kilichotokea kifuani kwake. Walisogea pembeni kidogo, kisha Pamela akajifunua shati lake na kujitazama kwa umakini. Wote hawakuamini kilichotokea kwani titi lake lilikuwa limerudi kama lilivyokuwa. Pamela alishtuka sana na kupiga kelele za shangwe huku akiruka kama ndama. Akamkimbilia baba yake na kumkumbatia kwa nguvu.
"Baba! Nashukuru baba! Asante!" Alisema Pamela kwa furaha kuzidi kiasi.
"No Pamela! Mshukuru Mungu sio mimi" alisema Baba Pamela huku akitabasamu.
Pamela alimuachia baba yake na kumfuata mama yake, chozi likamdondoka kwa uchungu huku akimkumbatia mama yake.
"Nisamehe sana mama! Naomba unisamehe kwa kukufanya ukose amani na kujisikia vibaya kwaajili yangu. Nakupenda sana mama.. Nisamehe mama!" Alisema Pamela huku akilia kwa uchungu.
"Pamela mwanangu! Usijali kwa yote yaliyotokea nilishakusamehe" alisema mama Pamela huku akimkumbatia kwa mahaba mazito binti yake mpenzi.
Baba Pamela alisimama pembeni yao kisha akapiga hatua za taratibu na kuwasogelea.
"Mke wangu... Familia yetu ingekuwa pabaya sana kwaajili ya yule adui! Lakini ni funzo kwako kuwa usimwamini kila mtu pia jifunze kumcha Mungu kwa moyo wote"
"Ashukuriwe Mungu sana! Tangu Leo wote tutamcha Mungu" alisema Mama Pamela.
"Kweli kabisa.. Mungu ni mkuu" alisema Pamela kisha Wote wakakumbatiana kwa furaha, ile furaha ya mwanzo ikawa maradufu. Kila mmoja alionekana kufurahi sana ule umoja uliotaka kuvurugika ukarejea tena katika familia ile ikazidi kung'ara na kuwa familia bora.
"Hakuna wa kumfananisha na Mungu!" Walisema kwa pamoja huku wakiwa na furaha ya ajabu.
*****
Leyla alipokea ugeni kutoka kanisani kwake ambapo wanamaombi watano walitia timu nyumbani kwake na kuiikuta familia ile ikiwa imepoteza furaha kabisa.
Leyla aliwakaribisha wageni wake vizuri na kuwakaribisha viti.
Mwalimu John na Judith walikuwa wapo kimya tu ingawa moyoni mwao walifurahia ujio wa watu wale.
Leyla akaamua kuwaambia kila kitu kilichotokea ndipo Walipoanza maombi yao. Walijtahidi kusali kwa imani kubwa sana. Baada ya maombi ya kama SAA zima ndipo maombi yao yalipoanza kujibiwa. Mambo ya ajabu yalianza kutokea ambApo mwalimu John alianza kuzungumza lakini cha ajabu funza walianza kutoka tena miguuni.
"Kuna mtu ni mchawi hapa" alisema Mwalimu John na kuwafanya wote wastaajabu.
"Tulia mume wangu watu wanakusaidia..." Alisema Leyla akimwambia mumewe.
"Nasema kuna Mtu anaroga hapa... Atoke.." Maneno hayo ya Mwalimu John yaliwafanya wote watazamane na kusitisha maombi kwa muda. Mwalimu John aliendelea kuongea.
"Wewe acha kuroga maombi ya wenzako... Wewe! Nikuseme?" Alisikika mwalimu John wakati huo wote walikuwa wameinamisha sura zao chini wakiogopa kutajwa. Baada ya dakika kadhaa kupita Mwalimu John alimsogelea mwanamke mmoja na kumshika bega.
"Sema ukweli la sivyo hawa funza wanahamia mwilini mwako.." Alisema mwalimu John huku akimkazia macho mwanamke yule.
"Mi..mimi..nime.. Mimi.." Alibabaika yule mwanamke.
"Ukidanganya tu funza wanakuhamia..."
"Ahm..aah.. Kweli.. Nilitaka..nilikuwa naroga msiendelee na maombi.." Alisema yule mwanamke akiwa anaona aibu kupita kiasi.
"Haya tokaa" aliamrisha mwalimu John na yule mwanamke akaondoka haraka huku kila mtu akimtazama kwa mshangao.
Hawakupoteza muda maombi yakaendelea na hawakutumia muda mrefu sana funza kwa mwalimu John wakapotea wote. Na mara ile Judith aliona ulimi wake ukiwa mwepesi sana na akaweza kuongea. Mwalimu John alikuwa kama aliyetoka usingizini alishtuka mno kuona kila kinachoendelea.
"Jamani.. Doreen ulitaka kuniua? Kwanini Doreen?" Alisema mwalimu John.
"Doreen ni nani?" Aliuliza mwanamaombi mmoja.
"Ni mwanafunzi wangu... Ni mchawi sana alitaka kuniua na alinifanyia mambo ya aibu sana" mwalimu John akasimulia kila kitu kuhusu Doreen.
Judithi pia akaeleza kila kitu kilichompata Mwalimu Jason ambaye tayari alishafariki dunia.
"Oh poleni sana watumishi Mungu ni mwema... Cha msingi mumrudie yeye!"
"Amen!"
Hatimaye mwalimu John na Judith wakarudia hali ya kawaida na furaha yao ikarejea tena. Walimshukuru sana Mungu.
Mwalimu John alimsogelea mkewe na kumbatia kwa dhati na upendo.
"Asante kwa upendo wako wa dhati uliokufanya uwe mvumilivu mno kwangu... Nakupenda!" Alisema mwalimu John na Leyla akatabasamu tu.
Wanamaombi wale walishukuru Mungu na kuwasihi familia ile pamoja na Judith kutomuacha Mungu. Kisha wakaondoka zao.
*****
Doreen alipokuwa anakimbia ndivyo kadri kipigo kilipomzidia. Kwani aliadhibiwa sana na Dorice na wakati huohuo Mungu alikmwadhibu kupitia maombi ya watumishi wake waaminifu.
Doreen alihisi mwisho wake umefika. Alilia kwa uchungu huku akipiga hatua za kichovu kuelekea nyumbani kwa kina Eddy kama Alivyoambiwa na Dorice ili akajisalimishe na kuombs msamaha.
Safari ilikuwa ndefu kwa binti yule aliyeuwa watu wengi shuleni kwao na kuwadhuru walimu wake wasiokuwa na hatia.
Hakuwahi kufika nyumbani kwa akina Eddy lakini alifika bila kupenda.
Umati wa watu uliokuwa nyumbani kwa mr Aloyce uliongezeka zaidi baada ya Doreen kufika pale.
Kulizuka hali ya tafrani katika eneo lile.
"Mimi ndo Maimuna halisi... Sio mama Eddy kama ulivyodhani.." Alisema Maimuna akiwa na sura mbaya kupita kiasi. Alikuwa ni mweusi mithili ya mkaa wa chunya, macho makubwa makali, mekundu kama pilipili, alikuwa na tumbo kubwa sana lililojaa michiriz, nywee zilikuwa chafu tena zimesokotana sana huku midomo yake mipana myeusi ikiyasitiri meno yake yaliyokaa hovyohovyo kinyani mwake.
Mr Aloyce aliishiwa nguvu, alishindwa kulia akadhindwa kuongea akabaki kimya amejiinamia.
Ujio wa Doreen na umati mwingine wa watu ukawa utata mwingine kwa Mr Aloyce.
"Nisamehe Eddy..." Alisikika Doreen akilia kwa sauti na wakati huo Eddy alikuwa anatembea taratibu kutokea ndani na kuja kymushuhudia kinachoendelea. Waandishi wa habari walikuwa wengi wakipiga picha tukio lile la ajabu.
Itaendelea....
RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 36 na 37
RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 36 & 37
MTUNZI:ENEA FAIDY
...Mama Eddy alitazama juu ili kuona kama kuna chochote lakini hakuona kitu. Ilimbidi atumie nguvu zake za uchawi alizokuwa Nazo ili kujilinda kwani aliziona dalili za kuvamiwa katika mazingira ya kutatanisha.
Mama Eddy ambaye jina lake halisi alijulikana kama Maimuna hakuwa Mtu wa kawaida Bali alitumwa na uongozi mkuu wa himaya aliyotokea Doreen ili kumsaidia kupata vitu alivyovihitaji.
Alitumia mbinu ya kujifanya mke wa Mr Aloyce ili kuweza kumteka vizuri na kumfanya asihangaike sana kuhusu mwanae kwani kulikuwa na uwezekano mkubwa sana wa kuharibu kazi. Maimuna alikuwa ni kijakazi mkongwe wa Bi Tatile na alikuwa akiaminika sana katika himaya ya Wanatatile kwani ni mtu pekee aliyewahi kufanikisha ajali kubwa ya mabasi mawili iliyoua abiria wote kisha wakafanywa kitoweo katika sikukuu ya kumpongeza Bi Tatile kama kiongozi bora wa wachawi wote Afrika Mashariki. Bi Maimuna alikuwa akiaminika sana kwa kila kazi anayoagizwa kwani hakuwahi kufanya makosa zaidi ya tukio moja tu la kuanguka kanisani akiwa katika harakati za kuwanga mchana.
"Maimuna! Maimuna! Hapa sio kwako na Leo ndio mwisho wa ubaya wako kwenye familia hii" ilisikika sauti nyororo isiyo na mkwaruzo hata kidogo huku ikijirudia rudia. Maimuna alibaki na mshangao wa ajabu sana, akataharuki huku akihema kwa nguvu. Akaaangaza macho kila upande pasipo kumuona mtu yeyote.
Akazidi kuchanganyikiwa sana. Ghafla wazo likamjia akilini mwake, bila kuchelewa akaamua kulifanyia kazi. Akanyoosha mkono wake wake wa kulia kisha nguvu nyingi zikamjia kama radi mkononi mwake. Bi Maimuna akaachia tabasamu mwanana akiamini hakuna kitakachomdhuru kwa wakati ule wala wakati mwingine wowote. akatulia kimya akimsubiri adui yake, lakini hakuona chochote zaidi ya ukimya mzito uliokuwa umetawala.
"Kumbe unaniogopa eeeh!" Alisema Maimuna.
"Ha ha ha! Sikuogopi Maimuna... Nakuvutia pumzi tu maana sina papara" sauti ile iliyojaa dharau ilisikika. Bi Maimuna hakutushika hata kidogo kwani alikuwa anajiamini kupita kiasi. Ghafla sura yake ikabadilika sana na kuwa sura ya kutisha sana.
Meno yakawa marefu kama mnyama mkali, kucha zikawa ndefu na Kali kama za chui anayemvamia swala, macho yake yakawa meusi huku mboni yake ikiwa nyekundu kama moto. Lengo lake lilikuwa ni kuonesha nguvu zake mbele ya adui yake ambaye hakujua ni nani. Ghafla kicheko kikali cha kutisha kilichojaa dhauri na jeuri kikasikika na kumfanya Maimuna ajione mdogo kama simimizi ilihali hamjui nana aliyemcheka.
Wakati huo huo Mlango ulifunguliwa na Mr Aloyce aliingia sebuleni pale.
"Mamaaaa" Mr Aloyce alipiga ukunga wa nguvu baada ya kumkuta mkewe akiwa na umbile la kutisha sana. Uvumilivu ulimshinda alijikuta anakimbia nje kama chizi huku akihema kwa nguvu. Mlinzi alimshangaa Mr Aloyce bila kuelewa kinachoendelea.
"Vipi bosi?" Aliuliza mlinzi huku akicheka sana. Mr Aloyce alianguka chini kama mzigo huku akihema kama Mtu aliyepanda mlima mrefu kwa kasi. Mlinzi alimsogelea na kumuuliza kilichojiri.
"Kuna maajabu humo ndani"
"Maajabu gani?"
"Mke.. Mke wangu...Ame..."
"Amefanyaje tena?" Aliuliza mlinzi kwa woga kwani alishapewa onto Kali na mwanamke yule kuwa asimfatilie kwa lolote. Lakini kabla hajasema chochote kuna kitu kiliwashtua Mr Aloyce na mlinzi wakabaki wameduwaa kwa mshangao.
******
Mama Pamela hakuwa na la kufanya zaidi ya kulia tu. Muda wote ule hakujua Doreen anaendeleaje ila kilichomshangaza ni kwanini Doreen hakwenda sebuleni kujumuika nao? Alinyanyuka kitini na kwenda chumbani kwake. Lakini ghafla mshangao wa ghafla ulimvaa mwanamama yule baada ya kukuta hali ya chumba ni mbaya sana kila kitu kilikuwa shaghalabaghala tu, ndipo machale yakamcheza, akasogelea droo anayohifadhia pesa.
"Mungu wangu!" Alishtuka mama Pamela baada yakukuta droo IPO wazi lakini haina pesa yoyote zaidi ya stakabadhi ambazo hakuwa na shida nazo wakati ule. Macho yalimtoka kwa mshangao huku akitoatoa vitu ndani ya droo ile bila kuona chochote. Akasimama wima akiwa ameshika mkono kiunoni kwa hasira
"Doreen!" Aliita kwa jazba bila kujua Doreen alikwishaondoka muda mrefu uliopita. Mama Pamela akakugua tena ili kujiridisha kama kweli pesa hazikuwamo lakini bado hakukuta pesa ndani ya droo ile wala eneo lingine chumbani mle.
Mama Pamela alichanganyikiwa sana akatoka ndani ya chumba kile na kupiga hatua za harakaharaka koridoni kuelekea chumbani kwa Doreen.
Alifika mlangoni na kufungua mlango kwa jazba kubwa. Lakini cha ajabu chumba kilikuwa kitupu na hakukuwa na mtu yeyote wala dalili za uwepo wa mtu. Mama Pamela akahamaki, akamwita Doreen kwa sauti kali lakini hakuitikia.
"Mungu wangu ina maana Doreen ametoroka na pesa au?" Alijiuliza Mama Pamela akiwa ameishiwa nguvu kabisa. Hakutaka kuamini kama binti anayemuamini kiasi kile angetenda tukio lililotokea.
Mama Pamela alitoka nje ya nyumba yake ili kumtazama vizuri Doreen. Alimtafuta pale uani na kila upande wa nyumba lakini Doreen hakuwepo. Moyo wa mama Pamela ukatawaliwa na lawama nyingi sana. Akajilaumu ni kwanini hakumsikiliza mumewe mpaka yote hayo yametokea.
Akakaa chini kibarazani huku machozi yakimchuruzika. Kila akikumbuka maneno ya mwanae roho ilimuuma zaidi, hakuwa na hamu hata ya kula. Alikuwa na simanzi nzito iliyopelekea mafuriko ya machozi usoni mwake. Alilia mpaka machozi yakamkauka akiwa pale pale kibarazani kwake. Hakutaka hata kumwona binti yake kwani uchungu ungemzidia. Kwa jinsi alivyokuwa akimpenda na kumjali Pamela hakuamini kirahisi kuwa Leo amekuwa adui yake mkubwa na kumpa lawama za uchawi.
"Mungu tu Anajua" aliwaza Mama Pamela.
Majira ya saa kumi na moja jioni, Baba Pamela aliwasili jijini Mbeya na kufika nyumbani kwake akiwa na mawazo tele juu ya familia yake. Alipofika ndani tu alikutana na mkewe ambaye uso wake ulivimba sana kwa machozi ya siku nzima. Baba Pamela hakushangaa sana kwani alihisi mkewe anamlilia binti yao Pamela kumbe si hivyo tu, Bali alikuwa na jambo zito lililomtatiza sana moyoni mwake.
****
Familia ya akina Dorice ikiwa bado imekaa kikao babu yake Dorice aliyefahamika kama Mganga Tawi La Mtawile alikuwa tayari ametoa wazo kuwa atafanya jambo.
Familia nzima ikaondoka kwenye nyumba ya mama Dorice na kwenda moja kwa moja kwa Mganga Tawi la Mtawile ili kujua Dorice yupo wapi na katika hali gani.
Na kwakuwa hapakuwa mbali sana, walitumia mwendo wa dakika tano tu mpaka kufika kwenye nyumba ta Tawi La Mtawile.
Mganga yule maarufu mkoani singida, alikuwa ametenga eneo maalum nyumbani kwake kwaajili ya shughuli za uganga. Alipanga vyema vibuyu na dawa zake pembeni alizungushia kaniki nyeusi na nyekundu. Akavua viatu, kisha akawaamrisha wote waliombatana nae wavue viatu ndipo wakae kwenye zulia alilotandika chini. Wote wakafata kama walivyoamriwa.
Mganga Tawi alianza kuimba nyimbo za kuita mizimu na kuongea maneno ambayo wengine hawakuyaelewa . alitumia dakika kumi nzima kisha akachukua kioo kikubwa, akanyunyiza dawa na kuipakaza vizuri kwa kutumia mkia kama wa ng'ombe. Akaita jina la Dorice Mara tatu. Baada ya muda mfupi ardhi ikatetemeka sana radi zikapiga mfulululizo na kuwafanya wote waogope. Na kila mmoja alitamani kukimbia kwani palikuwa na utisho wa ajabu....
Riwaya:Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) -:Sehemu ya 37
....ukimya mzito ulitawala huku ndugu zake Dorice wakijiuliza ni mini kitatokea. Ghafla moshi mweusi ulioambatana na radi ukatokea mbele yao karibu na mti mdogo uliokuwa karibu na kile kijumba cha uganga cha Tawi La Mtawile. Wote wakakaza macho kwa woga huku wakitazama kwa makini moshi ule ulitokana na nini ilhali hakuna moto wowote katika eneo lile.
Kwa namna ya ajabu na ya kustaabisha sana ambayo hakuna aliyeitarajia. Doreen alitokea mbele yao akiwa na muonekano tofauti na waliomzoea. Alikuwa ni mrembo kupita kiasi huku marashi makali yenye harufu nzuri yakizidi kuziumiza pua zao kwa fujo, mikufu ya dhahabu ilining'nia shingoni mwake ikienda sambamba na hereni ilizokuwa amezivaa pamoja na Pete kwenye vidole vyake. Kila mmoja alionesha mshangao wa ajabu kwani hawakuelewa ni kwanini Dorice yupo vile. Walitulia kimya huku woga ukiwazidia kwani walijua ni mzimu wa Dorice.
"Dorice umekuwa jini?" Aliuliza Tawi la Mtawile kwa sauti Kali. Dorice akajiweka sawa na kuachia tabasamu mwanana huku akipiga hatua chache kuwasogelea ndugu zake ingawa hakuwa nao karibu sana.
"Kwanza kabisa nimefurahi kuwaona ndugu zangu... Mama nilionana nae tangu akiwa kwenye basi.." Alisema Dorice kwa sauti tulivu sana. Maneno yake yalimshtua sana Mama Dorice na kumfanya akumbuke matukio yote yaliyomtokea alipokuwa kwenye basi na kabla ya kuingia kwenye basi.
"Ni wewe?? Kwanini umekuwa jini?" Alisema Mama Dorice kwa sauti iliyojaa woga sana.
"Mimi sio jini ila ninataka kulipa kisasi na kuwakomboa watu wasio na hatia.." Alisema Dorice.
Baada ya Dorice kusema vile Wote wakatazamana kwa mshangao sana, mama Dorice alitaman mwanae Arudi katika hali ya kawaida ili aendelee kuishi nae lakini Dorice asingekubali hata kidogo kupoteza malengo yake aliyopangilia kuyafanya kwa wakati ule.
"Mama ninakupenda sana! Nina imani nitarudi nyimbani baada ya kumaliza kazi yangu... Asanteni kwa kuniita... Kwaherini!" Aliema Dorice kwa huzuni kubwa huku neno kwaheri likijirudia Mara kadhaa mpaka Alipopotea na kutoonekana tena machoni mwao. Huzuni ikamtanda mama Dorice akamtazama Mganga Tawi la Mtawile na kwa bahati wakagongana macho kwa mganga pia alikuwa akimtazama mama Dorice.
"Baba Naomba mwanangu arudi.." Alisema Mama Dorice huku chozi likimlengalenga machoni.
"Mmh! Hilo haliwezekani mwanangu... Dorice hakuwa duniani Bali aliolewa na jini na amepewa nguvu za kijini ambazo ni tishio sana... Ni kubwa kuliko kawaida na nadhani kuna jambo muhimu amekuja kulifanya maana lasivyo asingerudishwa duniani... Tawii..Tawi La Mtawileeee..!"
Alisema mganga yule kwa sauti Kali ya kiganga.
"Inamaana atakuwa jini?"
"Inawezekana akawa MTU wa ujinini siku zote"
"Eeh Mungu wangu" alisema Mama Dorice.
Mganga hakuwa na la kufanya juu ya Dorice. Wanaukoo wote walistaajabu lakini hawakuwa na la kufanya zaidi ya kupigwa na butwaa. Mama Dorice alikuwa haamini kilichomtokea mwanawe lakini hakuwa na jinsi na maneno ya mganga yalizidi kumpa mawazo mengi.
Haukupita muda sana wote walitawanyika na kwenda majumbani mwao huku suala la Dorice likiwa gumzo akilini mwao.
****
"Mama Pamela unakumbuka nilikuambia nini kuhusu mgeni wako?" Aliuliza Baba Pamela.
"Nakumbuka mume wangu" alijibu mama Pamela huku akilia. Na alijua fika kwa jinsi Baba Pamela alivyompenda mwanae basi lazima atafanya kitu kulingana na tuhuma zile alizoshtakiwa na mwanae.
"Umeona maisha mlioishi tangu amekuja?"
"Ndio.. "
"Vizuri...hebu muite hapa.."
"Hayupo... Nimemtafuta sijamwona..." Alisema Mama Pamela huku aibu na hofu vikizidi kumvamia kwa kasi sana kwani usemi usemao Asiye Sikia La Mkuu huvunjika guu ulitimia kwake kwa wakati ule ingawa hakuwa na imani kama Aliyemtoa titi binti yake alikuwa Doreen.
"Hayupo? Ameenda wapi?"
"Sijui...sijuii ameto...ametoroka... Na pesa amechukua!"
"Umeona sasa mke wangu? Umeona faida za ubishi e??"
"Nisamehe mume wangu..."
"Nilishakusamehe ila nilikuacha ujifunze.. Ila roho inaniuma sana kwa binti yangu.." Alisema Baba Pamela kwa huzuni. Maneno yake yaliibua tumaini jipya kwa mama Pamela na yakawa faraja tosha kwake. Lakini Pamela akawa kikwazo sana kwake kwani bado alikazania msimamo wake kuwa mama yake ndiye aliyemroga na kuchukua titi lake.
"Pamela mwanangu... Mama yako hawezi kufanya hivyo isipokuwa mwanazaya yule asiye na haya... Nilimwona tangu alipifika hapa ya kwamba ni mchawi ila mke wangu hakuelewa... Alimwamini sana binti yule mwenye sura ya kondoo kumbe chui"alisema Baba Pamela kwa sauti iliyojaa busara ya hali ya juu.
"Unamtetea mama.."
"Simtetei ila utaujua ukweli tu... Naamini Mungu wa Mbinguni atafanya muujiza wake hapa na lazima aliyekutenda hivi adhalilishwe.. In Jesus Name" alisema Baba Pamela mwanaume aliyekuwa anamcha Mungu kupita kiasi, alikuwa ni mwaminifu sana katika masuala ya Mungu kupita kiasi.
*****
Mr Aloyce na Mlinzi walistaajabu sana baada ta kumuona Mama Eddy (maimuna) akitoka nje mbio akiwa hajavaa nguo yoyote huku akihema kwa nguvu na kupiga mayowe hovyo.
"Nimekosaaa! Nimekosaaa" alilalama Mama Eddy huku akianguka chini na kujigaragaza kama mtu anayecharazwa viboko na nyaya za umeme.
Mr Aloyce na mlinzi walibaki wakiwa wamepigwa butwaa. Kila mmoja alishindwa la kufanya zaidi ya kumtazama tu mwanamke yule aliyeendelea kupiga kelele sana.
"Sirudiiii!sirudiiii nasema..." Alizidi kupiga kelele.
"Bosi kwani mama ana nini?" Aliuliza mlinzi.
"Unaniuliza nini na wewe si unamuona?" Alijibu Mr Aloyce.
Mama Eddy alihangaika kwa muda mrefu pale nje. Mr Aloyce aliingia ndani na kuchukua upande wa khanga ili akamsitiri mkewe lakini kila alipotaka kumfunika mkewe alikimbia kama chizi pale nje hakutaka hata kujifunika kwani alikuwa akiadhibiwa kupita kiasi bila kumuona MTU aliyemwadhibu. Mr Aloyce ilibidi atulie tuli na kumuacha mkewe aendelee kutaabika kwani yeye hakuwa na la kufanya.
Baada ya muda mrefu kupita. Mama Eddy akaanza kutulia kidogo huku akihema kwa nguvu lakini aliongea maneno ambayo hakuna aliyemwelewa.
"Mke wangu kulikoni?" Alisema Mr Aloyce kwa huruma.
"Nisamehe"
"Nikusamehe nini?"
"Nisamehe Mr Aloyce"
Mama Eddy aliendelea kuomba msamaga bila kutaja kosa lake alilolifanya. Na akiwa amekaa pale chini ghafla akaendelea kuisikia sauti iliyokuwa inamwongelesha tangu alipokuwa ndani.
"Na hapo bado... Mpaka mlipie mateso mliyowatesa watu wasio na hatia" "sirudii tafadhali" alisema mama Eddy huku akipiga magoti.
Mlinzi Na Mr Aloyce walishindwa kumuelewa Mama Eddy kwani walihisi anazungumza peke yake .
"Hurudii nini?" Aliuliza Mr Aloyce.
"Naomba nikwambie ukweli baba Eddy...mimi....!" Alisema Mama Eddy.
Wakati huo mlinzi yule alikuwa akiwaza vitisho alivyotishwa na mwanamke yule pindi alipofika nyumbani pale.
'Mh kumbeee ni mchawii' aliwaza mlinzi.
"Ukweli upi" aliuliza Mr Aloyce kwa mshangao kwani katu hakujua kama kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia...
Itaendelea...
RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 35
RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 35
Mtunzi:Enea Faidy
......OOH siamini! Siamini kabisa kama sioni nyeti za Eddy" alisema Doreen akiwa amechanganyikiwa sana. Alitazama vizuri kwenye mkoba wake lakini hakuona nyeti za Eddy na hakujua nani amechukua. Kutokana na ulinzi mkali aliokuwa ameuweka ili kulinda vitu vile hakutaka kuamini kama Kweli vimeibiwa.
Doreen alikaa kitandani huku akifikiria kwa muda ndani ya chumba kile cha hoteli. Mawazo yake kila yalipofurika kichwani mwake,jasho jembamba lilimtiririka kwa kasi. "Mbona sielewi hii hali?" Alijiwazia huku akijaribu kutafuta tena nyeti zile ambazo kwake zilikuwa na thamani kubwa kuliko lulu. Doreen alikaa chini kwenye sakafu huku mawazo yakizidi kumuelemea.
Akavua nguo zote kisha akachukua mkoba wake na kuchukua kioo kidogo, akakipaka dawa ya ungaunga kisha akaanza kuomba dua kwa mizimu yake ili iweze kumsaidia katika janga lile gumu lililomkumba. "Mzimu wa Ngotongoto uliomkubwa sana katika ukoo wetu, Mtukufu Tatile na mizimu yako...
Tazama nilivyohangaika na kutafuta zawadi kubwa kama nilivyoagizwa lakini Leo hii sijui ni mzimu gani uliotokea na kutaka kunyang'anya kitu cha thamani kuliko dhahabu... Kafara iliyonzuri kwa mkuu wangu... Nihurumieni mja wenu! Naomba msaada wenu tafadhali.." Doreen alisema maneno Yale kwa hisia Kali huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini na mikono yake ikiwa imeshikilia kioo kile. " Ee mizimu yangu tukufu... Nisaidie kumjua mwizi wangu ili nimshughulikie..."
Alisema Doreen na ghafla radi Kali ikapiga kwenye kioo kisha kioo chote kikatapakaa damu. Doreen alishtuka sana akaona hali si shwari maana kioo kile kutapakaa damu kilikuwa na maana ya uwepo wa vita Kali dhidi yake. Hofu ikamtawala sana binti yule, hofu ikamtanda akashindwa kuelewa ni nani adui yake haswaa!. "Doreen! Doreen! Inakubidi kupambana!" Ilisikika sauti nzito yenye mwangwi mkali lakini mzungumzaji hakuonekana. "Doreen! Tumia nguvu zako zote ulizonazo, sisi tuko nyuma yako...
Onesha uwezo wako ili uutwae utukufu.. Uwe malkia uliyetukukaaa!!" Iliisisitiza sauti ile iliyoongea kwa msisitizo wa hali ya juu. Doreen aliogopa sana, akajua tayari mwisho wake umewadia lakini hakuwa na budi kujipa moyo wa ushindi na kuwa na matumaini ya kumbaini mbaya wake. "Nani mpinzani wanguuuu? Nasema nani atampinga Doreen Mbwana mtoto wa kitanga? Kama yupo ajeee!" Alisema Doreen kwa ujasiri wa hali ya juu na kuivua hofu yote aliyokuwa nayo.
Ghafla upepo mkali ukavuma kwa nguvu ndani ya chumba kile cha hoteli. Sauti Kali ya kicheko kilichojaa dharau na jeuri ikasikika na kumfanya Doreen ahamaki sana. Hali ya taharuki ikazuka moyoni mwa Doreen kwani daima hakufikiria kutokewa na mpinzani wa kumpinga mambo yake. "Doreen! Wakati wako umekwisha! Uchawi wako na mateso yako kwa wanadamu wasio na hatia sasa umefika kikomo... Ha ha ha nakwambia Doreen huna nafasi tena!"
Ilisikika sauti nyembamba na nyororo ikimwambia Doreen. Doreen alishtuka sana kusikia maneno Yale. Kilichomtisha zaidi ni kwamba alishindwa kumuona mtu aliyezungumza. "Kama una uwezo njoo nikuone!" Alisema Doreen. "Ha ha ha! Nitakuja unione wala usiwaze" maneno Yale yalizidi kumchanganya Doreen alibaki kimya akiwa ametumbua mimacho kama vitunguu huku akitazama huku na kule ndani ya chumba lakini bado hakufanikiwa kumuona mtu yule aliyezungumza kwa dharau sana.
"Naongea na huyu binti nilimfananisha na Dorice" alisema mama Dorice na kuwafanya majirani zake wageuke kumtazama Kwa mshangao. Hakujua watu wale wanashangaa nini lakini kilichowashangaza ni kwamba walimsikia mama Dorice akizungumza lakini hawakujua anaongea na nani kwani hawakumuona yule mtu. "Dada upo sawa?" "Nipo sawa ndio! Kwani vipi?" "Muda mrefu sana unaongea peke yako hapa..." "We Majaliwa tuheshimiane....
Nitaongeaje peke yangu kwani Mimi mwehu?" Alisema Mama Dorice kwa ukali kiasi. Abiria ndani ya gari ile walimshangaa sana mama Doreen wakahisi labda hayupo sawa kiakili kwani jirani yake kwenye siti hakuwa mwanamke Bali ni mwanaume mtu mzima mwenye umri kama miaka arobaini na tano.
Na kwa muda wote aliokuwa akizungumza Mama Dorice mwanaume yule alilala usingizi. "Dada hebu mtazame jirani yako vizuri" alisema Majaliwa. Mama Doreen alitamtazama jirani yake kwa makini sana. Ghafla akapatwa na mshtuko wa ghafla Baada ya kuona aliyedhani ni binti anayeendana sana na mwanaye si mwenye siti ile.
Aliyekaa pale ni mtu mwingine tofauti. Mama Dorice alishtuka sana, moyo ukampasuka paah! Hakuamini macho yake. "Kaka Majaliwa!" "Naam dada!" "Mbona sielewi Mimi? Ni mtihani gani huu?" "Labda una malaria dada?" "Sina chochote ila nilikuwa nimekaa na binti Fulani hapa. ." "Mmh! Hapo pagumu.." Mama Dorice alishindwa kuelewa chanzo cha yote hayo ikabidi akae kimya tu.
Macho yake yakatua dirishani na kutulia kwa muda kama aliyetazama kitu kilichomvutia sana. Ghafla akamwona Dorice dirishani( dirisha la gari) akimpungia mkono wa kumuaga kisha akaachia busu la mbali la upendo. Mama Dorice alishtuka sana akabaki ameduwaa tu mpaka Dorice alipopotea ghafla. "Kaka!" Aliita......
ITAENDELEA.....
RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 34
RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 34
Mtunzi:Enea Faidy
...Lakini cha ajabu kila alipomsogelea binti yule naye alikaza mwendo zaidi. Mama Dorice alishuhudia jinsi ambavyo mwanaye alitembea kwa madaha sana.
"Doriiiice!" Aliita kwa sauti lakini yule msichana alipogeuka hakuwa Dorice tena ilikuwa ni sura ya msichana mwingine kabisa. Mama Dorice alichanganyikiwa sana, ni kwanini hali inakuwa vile? Lakini hakupata jibu. Kaka yake alimfata haraka na kumshika mkono.
"Dada utagongwa na magari... Kwani unamfata nani?" Aliuliza kwa mshangao kwani yeye hakumwona MTU yeyote.
"Namfuata Dorice..."
"Huyo Dorice yuko wapi maana tangu tupo kule unamfuata tu?"
"Sio yeye.. Nimemfananisha...."
"Dada bwana usiwaze sana.... Ona sasa mpaka watu wanakushangaa ujue.. Unaita kila mtu Dorice..."
"Lakini Mimi nilimwona kabisa kaka...."
"Haya tuondoke"
Mama Dorice alikuwa bado anaifikiria ile hali, akajua lazima kuna kitu kinaebdelea kuhusu Dorice, kwanini amfananishe kiasi kile lakini bado hakuwa na jibu sahihi.
Wakati wa safari ulipowadia, waliingia kwenye basi na kukaa kwenye siti zao.Walisafiri kwa mwendo kidogo, ndipo macho ya mams Dorice yalipotua kwenye sura ya yule binti aliyemwona toka wakiwa kituo cha mabasi Jana yake. Na alikuwa amevaa nguo zile zile, alikaa Pembeni yake. Moyo ulimpasuka kwa mshtuko akafikinya macho yake na kumtazama tena binti yule aliyeachia tabasamu mwanana. Akamsalimu mama Dorice. Mama Dorice alishangaa, kilichomshangaza zaidi ni kwamba alipoingia kwenye gari hakumwona MTU yule na hata alipokaa hakukaa na binti yule. Sasa imekuaje yupo nae?
"Mama nilikuona sehemu!"
"Mh hata Mimi nilikuona!" Alisema mama Dorice.
"Kwanini ulikuwa unanifata?" Aliuliza binti yule ambaye kila wakati alipenda kutabasamu.
"Nilikuwa na kufananisha na mwanangu" alisema mama Dorice.
"Mwanao? Anaitwa Dorice?"
"Ndio... Umemjuaje?"aliuliza mama Dorice lakini msichana yule alicheka sana kitendo kilichomshangaza mama Dorice.
"Mama we si uliniita Dorice?"
"Eeh ndo jina lake.." Wakati wakiendelea na mazungumzo Yale mjomba wake Dorice alimshangaa sana dada yake.
"Dada mbona unaongea peke yako? Unajibizana na nani?"
******
Mama Pamela alimtazama binti yake na kumsikiliza kwa umakini.
"Niliota nipo hapa sebuleni... Halafu nikakuona wewe ukiwa haujavaa nguo... Ukanifata na kunishika kifuani kwa muda kisha ukaniachia.... Halafu ulikuwa unatisha sana usoni...." Alisema Pamela.
Mama Pamela hakutaka kuamini kile alichokisikia, alipigwa na butwaa sana na kubaki kinywa wazi akimshangaa mwanaye.
"Mimi? Pamela! Mbona sikuelewi?"
"Ndio mama nilikuona wewe ukichukua titi langu.. Mama kwanini umenifanyia hivyo?" Pamela alisema kwa msisitizo huku akilia. Mama Pamela alizidi kuchanganyikiwa maana hakutegemea kusikia maneno Yale kutoka kwa mwanaye.
"Ina maana unataka kusema mimi ni mchawi? Pamela kweli unanisingizia hivyo?" Mama Pamela alikuwa haamini lakini hivyo ndivyo Pamela alivyoota. Kwani wakati Doreen akichukua titi lake, pamela hakuiona sura ya Doreen ila alions sura ya Mama yake hivyo aliamini kuwa mama yake ndiye aliyemfanyia vile.
"Mama! Sikujua kuwa wewe ni mchawi! Kumbe ndivyo ulivyo? Nilikuamini sana mama yangu... Kwanini umenifanyia hivi? Kwanini mama?" Alilalama Doreen na kuonesha ni jinsi gani alivyopoteza uaminifu tena kwa mama yake. Ilikuwa vigumu sana kwa Mama Pamela kumuamisha mwanaye kuwa sio yeye aliyefanya kitendo kile cha ukatili.
"Pamela mwanangu... Wewe ndo mwanangu wa pekee, sina mtoto mwingine zaidi yako Leo hii mimi nikufanyie hivyo? Haiwezekani..." Alijitetea mama Pamela.
"Lakini mama... Ili yote yaishe lazima unirudishie titi langu... Na usipofanya hivyo nampigia simu baba namwambia kila kitu.... Na sio baba tu nawaambia ukoo mzima..."
"Pamela... Sio mimi mwanangu... Nisemeje unielewe?" Mama Pamela alijitahidi kujitetea kadri awezavyo lakini bado ilikuwa vigumu kueleweka. Pamela alilia sana huku akimbebesha mama yake mzigo wa lawama. Alichukua simu na kumpigia baba yake, hofu ikamvaa mama Pamela akiifikiria aibu kubwa ambayo angeipata kwenye ukoo wake na wa mumewe. Mpaka muda ule hakujua kinachoendelea kwa Doreen, kwani alidhani yupo chumbani kwake bila kujua Doreen alishaondoka muda mrefu. Kibaya zaidi kilichompa hofu ni kwamba mumewe angeamini maneno ya Pamela kutokana na jinsi mama Pamela alivyokuwa akimtetea Doreen.
"Lazima aamini... Na atajua ni kweli nimefanya hivyo ndio maana nilimkatalia sana Doreen... Haya majanga ya kupewa uchawi wakati mimi so mchawi!" Aliwaza mama Pamela bila kujua hatma ya tatizo lile.
"Daddy!" Alisema Pamela baada ya simu kupokelewa.
"Yes Pamela... Eti nini kimekupata mwanangu...?" Aliuliza Baba Pamela. Pamela akaongeza kilio huku akimtazama mama yake.
"Daddy! Fanya haraka uje... Kuna mambo mazito sana baba.. " alisema Pamela.
"Nakuja Leo jioni na ndege...."
"Uje tu baba yangu... Uje haraka.." Alisema Pamela huku akishindwa kuyazuia machozi yake.
Mama yake alibaki kimya huku machozi yakimdondoka. Alishindwa afanyeje.
"Unalia nini na huo uchawi wako?" Alisema Pamela kwa hasira huk
Oy...
ITAENDELEA.....
RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 32 na 33
Mtunzi:ENEA FAIDY
.... Shule ya sekondari Mabango ilikuwa na utulivu wa hali ya juu tangu Doreen alipoondoka shuleni pale. Licha ya kwamba kulikuwa na upungufu wa walimu lakini hali ilikuwa shwari kabisa. Wanafunzi waliendelea na masomo yao kama kawaida huku wakimshukuru Mungu kwa kuwaondolea mbaya wao aliyeisumbua shule ndani ya muda mfupi tu.
Majira ya saa saba mchana katika shule ile alifika Mwanaume mmoja wa makamo akiwa ameambatana na mwanamke mmoja mwembamba mrefu. Wanafunzi wa shule waliokuwa karibu waliweza kugundua kuwa mwanamke yule bila shaka alikuwa ni mama yake Dorice kwa jinsi walivyofanana. Nadia Joseph aliyekuwa anapita eneo lile la ofisi aliwasalimia kwa heshima kisha akasimama kidogo huku akitafakari jambo alilotaka kuzungumza.
"Samahani mama.. We ni ndugu yake Dorice.." Aliuliza Nadia huku akitabasamu.
"Ndio.. Ni mama yake mzazi.." Alijibu mama yule.
"Oh mmefanana sana... Vipi lakini hajambo?" Aliuliza Nadia akiwa anatabasamu lakini swali lile lilikuwa kama mwiba mkali moyoni mwa Mama Dorice kwani ujio wake pale shuleni ilikuwa ni kumfuata Dorice na kupata taarifa zake kwani ulipita muda mrefu sana bila mawasiliano yoyote.
"Kwani Dorice hayupo hapa shule?" Aliuliza Mwanaume aliyeambatana na Mama Dorice kwa mshangao. Na huyo alikuwa ni mjomba wa Dorice.
"Ah! Unataka kuniambia hayupo nyumbani?" Alishangaa Nadia lakini ndani ya muda mfupi alitokea madam Amina eneo lile hivyo Nadia aliamua kuondoka ili kukwepa adhabu.
Madam Amina aliwasogelea wageni wale na kuwasalimu. Kisha akawakaribisha ofisini. Bila kuchelewa wageni wale waliambatana na Mwalimu Na kuingia ofisini.
"Karibuni sana.. "
"Asante.. Sisi ni wazazi wa Dorice na tumekuja hapa kuuliza binti yetu anaendeleaje?"
"Dorice.. Alikuwa kidato cha nne?" Aliuliza mwalimu.
"Ndio!"
"Mmh! Mbona aliacha shule na tuliwapigia simu mkasema amefika" alisema Mwalimu Amina kwa mshangao. Kauli ile iliularua moyo wa mama Dorice na kumfanya achanganyikiwe sana, maana hakuna simu aliyopigiwa wala Kuambiwa chochote kuhusu mwanae.
"We mwalimu umechanganyikiwa? Mbona kama hujielewi eti?" Mama yule wa kinyaturu aliinuka kitini na kuanza kumfokea mwalimu.
Mwalim Amina aliamua kujitetea kwani hali ya hewa ilianza kuchafuka ofisini mle. "Tunamtaka mwanetu.. Mmemtorosha nyie? Au mmemuua?" Alizidi kucharuka mama Dorice.
Mwalimu Amina alikumbuka mbali, akakumbuka siku ambayo Dorice alipotea kisha wakapewa taarifa za upotevu wa mwanafunzi huyo. Barua ya maelezo iliandikwa kisha walimu wakapiga simu kwa wazazi wa Dorice. Lakini kwa bahati mbaya sana simu ilipokelewa na jini Mansoor kwa namna ya ajabu sana. Na jini huyo aliongea sauti ya Mama Dorice na kuwafanya walimu wajiaminishe vizuri kuwa waliongea na mama Dorice lakini kumbe haikuwa hivyo na hakuna aliyejua siri hiyo zaidi ya Mansoor pekee.
"Mama tena nilipiga simu Mimi.. Na ulikubali mwanao aache shule.." Alijitetea madam Amina lakini hakueleweka.
Wazazi wa Dorice waliondoka kwa hasira sana shuleni pale huku wakiwa hawajui binti yao alienda wapi. Roho iliwauma sana lakini hawakuwa na jinsi. Waliondoka na gari yao waliokuwa wamekodi ikawafikisha kituo cha mabasi Iringa mjini.
Walishuka ili watafute sehemu ya kula chakula kwani hawakula chochote tangu asubuhi kisha wakate tiketi, ghafla kwa mbali sana Mama Dorice alimwona msichana kama Dorice. Alijifuta macho yake na kutazama vizuri akamtazama vizuri binti yule.
"Kaka Dorice yule pale"
"Yuko wapi?" Kaka yake alishtuka sana.
"Pale mbele kwenye watu wengi.. Tumfate haraka.." Alisema Mama Dorice akiwa tayari ameanza kupiga hatua kuelekea kule alipo msichana yule.
********
"Chukua hii" Bi Tatile alimpa hirizi moja Doreen. Doreen aliipokea kwa mkono wake wa kushoto na kusikiliza maelekezo kwa umakini kutoka kwa Bi Tatile.
"Hii umeze sasa hivi.... Haraka sana.." Aliamrisha Bi Tatile na Doreen alifanya hivyo haraka. Akaibugia mdomoni na kuimeza. Alihisi maumivu makali sana ya Tumbo, akapiga kelele kwa kulalama.
"Hapa inabidi urudi haraka nyumbani... Ukajisaidie haja kubwa sebuleni kwenye sahani safi.. Kisha uzunguke sebuleni Mara Saba kutokea kona moja hadi nyingine huku akitamka jina la msichana yule... Umenielewa?"
"Nimekuelewa mtukufu.." Alijibu Doreen kwa woga kiasi.
"Haya ondoka haraka.." Aliamrisha Bi Tatile huku akimalizia na kicheko kikali cha kutisha.
Bila kuchelewa Doreen aliopotea eneo lile na kutokea nyumbani kwa Mama Pamela. Pindi alipokuwa anaingia ndani kilisikika kishindo kizito sana. Doreen aliingia ndani na kupulizia dawa ya kuwalaza usingizi wote waliokuwa ndani kisha akaenda sebuleni. Akachukua sahani nzuri sana Kabatini, akaiweka chini na kujisadia haja kubwa yenye harufu Kali sana kwenye sahani ile. Kisha akaenda kwenye kona ya kwanza na kuanza mzunguko wa kwanza huku akitamka jina la Pamela.
Akamaliza mizunguko saba kama alivyoambiwa punde Pamela alitokea sebuleni pale. Doreen alicheka kicheko kikali sana cha kutisha, huku akimsogelea Pamela aliyekuwa ameinamisha kichwa chino bila kumtamzama Doreen.
Doreen alisigeza mkono wake na kuusogeza kifuani kwa Doreen kwenye titi lake la kushoto. Akalishika titi lile huku akitamka maneno Fulani kisha titi lile likapotea kifuani kwa Pamela akabakiwa na titi moja tu. Pamela alikuwa hajielewi kabisa akiwa pale. Baada ya titi kuchukuliwa akapotea. Na Doreen pia akapotea huku moyoni mwake akifurahia ushindi alioupata kwani tayari kazi iliyomleta ilikuwa imekamilika.
Asubuhi na Mapema, Mama Pamela aliamka usingizini akiwa mchovu sana. Alijikongoja na kwenda chumbani kwa mwanaye alikuta amelala fofofo, akamshtua.
"Mbona umelala sana Leo?"
"Mama naumwa sana." Alisema Pamela kwa sauti ya kichovu.
"Unaumwa? Unaumwa nini? " mama Pamela alishangaa.
"Kifua kinaniuma sana.. Titi linauma balaa.."
"Titi?" Alishtuka mama Pamela.
"Ndio.."
"Pole sana.. Halafu kuna harufu naisikia humu ndani.. Sijui pua zangu.." Alisema mama Pamela na kulipuuza suala la binti yake kwani alihisi ni ugonjwa wa kawaida tu.
"Hata Mimi naisikia..." Alisema Pamela.
"Ngoja niangalie angalie basi huko sebuleni." Alisema Mama Pamela na kwenda sebuleni. Alipoingia tu alikaribishwa na harufu mbaya sana iliyomfanya apige chafya. Na kwa ukali wa harufu ile alitamani atapike. Macho yalitua moja kwa moja mpaka kwenye sahani yake iliyokuwa imejaa kinyesi pale sebuleni kwake.
"Oh My God!" Alishtuka Mama Pamela huku macho yamemtoka kama yai la kisasa.
"Ama kweli dunia ina mambo.. Pamelaaa! Njoo!" Alisikika mama Pamela.
Pamela aliitika na ndani ya sekunde chache alifika sebuleni pale.
"Oh gash! Nani kafanya ivi?" Alishangaa Pamela baada ya kushuhudia tukio lile pale sebuleni.
"Shangaa wewe! Maana mie nimeishiwa nguvu kabisa!" Alisema mama Pamela. Walishangaa kupita kiasi na muda si muda Doreen alifika sebuleni sebuleni pale na kuungana na wenye nyumba kushangaa tukio zima.
"Alaaniwe sana aliyefanya tukio hili.." Alisema Doreen huku akipiga makofi ya mshangao.
"Halafu Dada Pamela hapo kifuani pakoje?" Aliuliza Doreen.
Pamela alishtuka kusikia swali lile. Akajiangalia kifuani kwake na kugundua kifua chake kimetuna upande mmoja lakini upande mwingine hauna kitu. Hofu kuu na mshangao vikamvamia akajifunua shati na kujikagua zaidi.
*********
"Mama Eddy.. Nashukuru sana mdogo wangu kwa ulichonifanyia... Mungu tu ndo anaejua.... Kwaheri." Alisema Dada yake mama Eddy na kutoka sebuleni Pale.
Mr Aloyce alijtahidi kumzuia asiondoke ilishindikana. Mwanamke yule aliondoka kistaarabu na kuwaachia nyumba yao.
"Mke wangu ulichofanya sio ustaarabu.." Alisema Mr Alloyce.
"Ustaarabu haulipwi... Kwahiyo hauna faida.." Alijibu mama Eddy na kukaa kitini.
"Mh! Sawa..."
"Hebu tuachane na yaliyopita kuna jambo nataka nikuambie.
"Mama kwanini umefanya vile? Mbona umebadilika sana?"
"Na wewe sitaki kelele... Hebu ondoka hapa niongee na mume wangu.."
"Sawa lakini mamkubwa alikuwa tatari kunisaidia tatizo langu" alisema Eddy.
"Ulimwambia sio?"
"Ndio..." Alijibu Eddy kwa hasira na kutoka sebuleni pale akiwaacha na mazungumzo yao. Roho ilimuuma sana Eddy kwa kitendo alichofanya mama yake, lakini hakuwa na jinsi.
"Nisikilize mume wangu mpenzi.." Alisema ma Eddy.
"Sema"
"Nataka tumrudishe Eddy shuleni... Maana masomo yanampita sana.."
"Unasemaje? Vipi kuhusu tatizo lake?"
"Hilo lishakuwa la maisha cha msingi arudi shule"
"Hapo sijakuelewa mke wangu.. Si ni bora tumpeleke hata kwenye maombi?" Alisema Baba Eddy na katika vitu alivyovichukia mama Eddy yule wa bandia ni suala la maombi.
"Maombi kitu gani? Unawaamini wachungaji wenyewe waongo tu? Sitaki maombi kwa mwanangu asije akatupiwa majini bure..." Alisema mama Eddy.
"Kuombewa ataombewa tu... Tena nimekumbuka kitu..." Alisema Mr Aloyce na kunyanyuka kitini pale haraka..
SEHEMU YA 33
...BAADA ya kujikagua kwa muda Pamela aligundua hana titi lake moja la kushoto. Jasho jembamba lilimtiririka kwa kasi ya ajabu. Hakutaka kuamini kile alichokiona, akaanguka chini ghafla na kupoteza fahamu. Mama Pamela alipigwa na butwaa la ajabu, uvumilivu ukamshinda akamwita Pamela Mara kadhaa lakini Pamela hakuitikia. Kwa mshtuko alioupata pia mama Pamela alidondoka chini Puuh! Kama mzigo na kupoteza fahamu palepale.
Doreen alisimama pembeni yao, alicheka kwa kiburi sana kisha akaondoka zake sebuleni na kuingia chumbani kwa mama Pamela moja kwa moja. Aliingia chumbani kinyumenyume kisha akatamka maneno Fulani halafu akageuka na kusogelea kitanda cha Mama Pamela, akatazama chumba kizima kisha akagundua sehemu yenye pesa. Akatikisa kichwa na kuisogelea droo moja ya 'dressing table' na kuchukua pesa zote zilizokuwemo mle. Na droo ile ndio ambayo aliitumia mama Pamela kuhiffadhi pesa zote.
Bila huruma Doreen alichukua pesa zote alizozikuta mle, zilikuwa takribani laki tano kisha akaenda chumbani kwake na kubadili nguo haraka kisha kisha akachukua begi lake dogo akaondoka zake.
Doreen alitembea mwendo wa haraka sana mpaka alipofika barabarani na kupanda daladala inayoelekea stendi kuu ya Nanenane.
Mama Pamela na mwanaye walilala pale chini kwa muda wakiwa hawajitambui. Ndani ya nusu saa nzima ndipo mama Pamela alipopata fahamu na kuwezs kuinuka, alikaa dakika tano nzima ndipo kumbukumbu zikamrejelea. Machozi yalimdondoka huku akiinuka na kwenda kuchukua simu kitu cha kumpepea mwanae ili azinduke. Alichukua khanga laini na kuanza kumpepea Pamela mpaka alipozinduka. Lakini muda wote huo kuna kitu alikifikiria na alihisi kimepungua mle ndani. Akawaza kwa muda ni kitu gani hicho ndipo akakumbuka kuwa hakumwona Doreen.
"Doreen! Doreen!" Aliita mama Pamela lakini hakusikia sauti yoyote iliyoitikia. Akaachana nae akijua labda yupo nje.
"Mama siamini! Sitaki kuamini kilichonitokea!" Alisema Pamela huku akilia.
"Sijui nani amefanya hivi?" Aliuliza mama Pamela.
"Mama! Kuna ndoto niliota... Ila sikudhani kama ni kweli kumbe ilibeba ukweli mzito sana!" Alisema Pamela kwa huzuni huku akilia.
"Ndoto gani hiyo? Na je ulimwona Mtu yeyote?"
"Ndio mama nilimwona!"
"Alikuwa nani?"
Kabla Pamela hajasimulia chochote kuhusu ndoto aliyoota, simu ya Mama Pamela iliita na kumfanya ainuke haraka na kwenda kuifata simu yake. Mpigaji alikuwa ni Baba Pamela, mama Pamela alipokea simu huku huzuni ikimzidia.
"Haloo mume wangu..."
"Halloo... Habari za huko?"
"Mmh.. Za huku si nzuri...!"
"Mh! Kwanini?" Alishtuka baba Pamela. Mama Pamela akamsimulia kila kitu kilichotokea nyumbani kwake tangu alipoondoka. Mkasa ule mzito ulimshangaza sana Baba Pamela, alikuwa haamini kabisa kilichomtokea binti yake.
"Ina maana Pamela hana titi moja sasa?"
"Ndi..ndioo..."
"Unaona sasa mke wangu? Nilikwambiaje Mimi?? Nilikwambia nini kuhusu yule mgeni wako?" Baba Pamela alianza kumlaumu mkewe kwa kutokuwa mwelewa lakini suala lile likazua ubishi kwa mama Pamela kwani hakuamini kabisa suala la Doreen kuhusika ns ushirikina.
"Mume wangu... Unamkosea Mungu kumhusisha yule binti na ushirikina, yule mtoto ni mpole tena mstaarabu.." Alisema mama Pamela.
"Tatizo lako mke wangu ni hilo... Hutaki kuukubali ukweli na ndio maana umesababisha matatizo kwa mwanangu bora yangekukuta we we.." Alisema Baba Pamela.
"Baba Pamela mbona we king'ang'anizi hivyo? Doreen sio mchawi... Waliofanya hivyo watakuwa ni majirani tu..."
"Mh umenishinda we mwanamke." Baba Pamela alikata simu kwa hasira.
Akili ya Mama; amela ilikuwa ngumu sana kuamini maneno ya mumewe. Alijua mumewe anamsingizia tu binti wa watu, mtoto mwenye adabu kupita kiasi, mchapakazi tena mwenye hekima. Hivyo ndivyo mama Pamela alivyomchukulia Doreen bila kujua upande wa pili Doreen alikuwa ni mtu wa aina gani.
"Hebu nisimulie vizuri hiyo ndoto yako Pamela.."
"Mama tuondoe kwanza hicho kinyesi maana harufu yake inanisumbua sana..." Alisema Pamela.
Mama Pamela alienda jikoni na kutafuta mifuko ya plastiki kisha akajivalisha mikononi halafu akaenda kubeba ile sahani yenye uchafu kutoka tumboni mwa MTU mwingine na kuubeba kwa kinyaa sana kisha akaenda nao nje. Alitafuta eneo zuri na kuchimba shimo dogo akafukia uchafu ule pamoja na sahani. Alinawa mikono kisha akarudi tena sebuleni ambapo bado palikuwa na harufu Kali. Akawasha kiyoyozi na kufungua madirisha yote kisha harufu ile ikaanza kuaga Nyumba taratibu sana na kwa maringo yaliyokithiri.
Baada ya kuhakikisha usalama wa nyumba yake mama Pamela akaketi kitini na kumsikiliza mwanaye.
****
Baba Eddy alisogelea droo yake ya kuhifadhia vitu na kuchukua kijidaftari kimoja kidogo amabacho Mara nyingi alikitumia kuhifadhia namba za simu za watu wake muhimu. Baada kukipata alienda nacho sebuleni na kuketi kitini huku akikipekuapekua kwa uangalifu.
"Nimefanya uzembe kwa muda mrefu lakini sasa nimegundua njia sahihi ya kumtibu mwanangu..." Alisema Mr Aloyce.
"Kwani njia gani umeigundua? Kuna daktari unamfahamu?" Aliuliza mama Eddy.
"Kwahili suala halihitaji daktari..."
"Mh kivipi... Basi mganga...!"
"Mganga wa nini? Umesahau kilikutokea tulipotaka kwenda kwa mganga?" Alisema Baba Eddy huku akizinakiri namba Fulani kutoka kwenye kile kijidaftari na kuweka kwenye simu yake.
"Mbali na hao... Unafikiri nani atatusaidia mume wangu? Hakuna mwingine... Tusipoenda kwa daktari basi ni kwa mganga tu.." Alisema mama Eddy kwa sauti ya ushawishi sana lakini haikumwingia akilini hata kidogo baba Eddy.
"Hao uliowasema watashindwa... Cha msingi ni kumtegemea Mungu tu..."
"Unampigia Mchungaji?" Alishtuka mama Eddy.
"Ndio.." Aliitikia Baba Eddy na tayari muda huo huo alipiga simu na ikaanza kuita.
"Wewe mbona upo ivo? Mchungaji wa nini sasa? Hatokusaidia kitu zaidi ya kupoteza muda.. Hebu kata simu.." Alisema mama Eddy huku akimnyang'anya simu mumewe na kukata. Baba Eddy alimshangaa sana mkewe. Alijikuta anamtandika Kofi zito sana la usoni bila kutarajia.
"We mwanamke ni mchawi nini? Kwanini ukatae maombi ya watu wa Mungu?" .
Mwanamke yule alipiga ukunga kwa maumivu. Akajishika shavu lake kwa kuugulia kipigo kile.
"Unanipiga Mimi?" Alisema mama Eddy. Mr Aloyce alibaki kimya tu bila kusema neno kwani alikuwa na hasira sana. Alichukua simu yake na kuondoka sebuleni pale, akaingia chumbani. Haukupita muda kabla hata hajapiga simu tena mama Eddy aliingia chumbani.
"Si umenipiga? Sawa! Wewe ni mbabe! Ila nitakuonesha!" Alisema Mama Eddy na kuzidi kumtia hasira zaidi Mr Aloyce.
"Sitaki masikhara kwenye vitu vya msingi ondoka huku chumbani!" Alisema Mr Aloyyce huku akijaribu kupiga tena simu.
"Mume wangu... Nisamehe basi... Tuyamalize basi baby!" Alisema mwanamke yule kwa sauti ya mahaba utadhani sio yule aliyekuwa na hasira hapo mwanzo. Alimsogelea mumewe kimahaba na kumyang'anya simu mumewe kisha akamteremshia mvua ya mabusu mdomoni mwake.
"Nakupenda mume wangu..." Alisema mwanamke yule akiwa amekata simu na kuiweka pembeni. Mr Aloyce alibaki kimya akimtazama tu mkewe kwa mambo anayoyafanya. Mwanamke yule aliendelea kumpapasa mumewe akiwa na lengo la kumfanya Mr Aloyce apoteze wazo la kumpigia simu mchungaji. Kwani alifahamu vizuri nguvu ya maombi ya watu wa Mungu na jinsi ambavyo angeshindwa kufanya kazi yake.
Licha ya kutumia mtego ule kwa Mr Aloyce lakini bado ilishindikana kumfunga akili yake ya kumpigia simu mchungaji. Mr Aloyce alisukuma kwa nguv na kuchukua simu yake kisha akaenda chumba cha wageni na kujifungia mlango, akampigia simu mchungaji. Alipopokea tu simu ile, ghafla mlango wa chumba ukafunguliwa. Mr Aloyce alishtuka sana, kwani alikuwa amefunga mlango na funguo. Mkewe aliingia.
"Mchungaji.. Naitwa Mr Aloyce... Nina matatizo makubwa sana kwenye familia yangu nahitaji maombi mchungaji tafadhali..."
Alijieleza mr Aloyce kabla hata ya salamu. Lakini muda huo alisikia sonyo Kali sana kutoka kwa mkewe, na hakuelewa ni kwanini mkewe alisonya kidharau kiasi kile kisha akatoka chumbani mle.
*****
Mama Dorice alitembea mwendo wa haraka sana na kumkaribia msichana yule aliyedhani kuwa ni mwanaye. Alimkaribia msichana yule na kumwita "Dorice!" Msichana yule akageuka na kumtazama aliyemwita ndipo mama Dorice aliposhtika sana baada ya kugundua binti yule hakuwa Dorice.
"Samahani binti nimekufananisha.." Alisema mama Dorice na kumgeukia kaka yake ambaye alikuwa anamfata kama Bendera inayofuata upepo.
"Dada mbona sikuelewi..?" Aliuliza mjomba wake Dorice.
"Kaka acha tu...."
"Kwani vipi?"
"Nilimwona Dorice kabisa lakini nilipofika hapa kumbe sio...."
"Umemfananisha?"
"Nadhani..."
"Haya twende basi tukate tiketi... Turudi nyumbani tuangalie ni jinsi gani ya kumpata mwanetu.... Maana hatuwezi sema alifariki bila uchunguzi labda aliacha shule akaolewa?"
"Ila sidhani kama inawezekana Dorice aolewe kizembe ivo... "
"Usikatae dada yote Yanawezekana..." Alisema mjomba.
Waliondoka eneo lile na kwenda moja kwa moja kwenye mgahawa mmoja ambapo walipata chakula kisha wakaenda kukata tiketi ya basi. Walipokuwa pale , mama Dorice alimwona tena MTU kama Dorice akiwa amevaa mavazi Yale yale kama ya yule aliyemwona mwanzo.
Mama Dorice alishtuka. Akamtazama kwa makini binti yule akagungua ni yeye kabisa tena cha ajabu binti yule alimpungia mkono huku akitabasamu. Na alikuwa amependeza kupita kiasi gauni refu jekundu alilovaa, pamoja na viatu virefu vya bluu alivyovaa vilivyoenda sambamba na mkufu na hereni zake. Huku nywele zake ndefu zilizojimwaga zikimfanya aonekane maridadi zaidi.
Mama Dorice hakulaza damu akaamua kumfuata haraka binti yule lakini cha ajabu
ITAENDELEA.....
RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU 31
Mtunzi:ENEA FAIDY
...Doreen alimsikiliza kwa Umakini mama Pamela ili ajue ni swali gani analotaka kuuliza. Mama Pamela alikaa vyema kisha akakohoa kidogo na kumtazama Kwa makini Doreen.
"Niulize Tu mama" alisema Doreen.
"Hivi ni kitu gani unapenda nikufanyie ili moyo wako ufurahi? Maana nimependa sana heshima na adabu uliyojaaliwa." Alisema mama Pamela.
"Kiukweli mama Mimi napenda sana unitafutie shule.. Ili niweze kusoma na kufikia malengo yangu" alisema Doreen.
"Shule tu? Wala usijali wiki ijayo nitakuwa tayari nimetafuta shule kwa ajili yako.."
"Nitafurahi sana mama..."
"Unapenda shule ya kutwa au bweni?"
"Yoyote tu itanifaa" alisema Doreen.
Suala lile lilimfurahisha sana Doreen, aliendelea kuishi kwa kunyenyekea sana ndani ya nyumba ile, lakini katika ulimwengu mwingine alikuwa ni mtu jeuri na katili kwa familia ile. Kila Mara aliliwinda sana titi la Pamela, alitamani kulipata kwa udi na uvumba lakini kwa bahati mbaya ilikuwa vigumu kulipata. Alitumia kila namna lakini bado hakuelewa sababu ya kushindwa kulipata titi la Pamela.
Hasira zilimuwaka sana Doreen pale alipoingia chumbani kwa Pamela usiku na kutaka kumkata titi lake. Alikuta Pamela amelala usingizi mzito sana, akampulizia dawa ili usingizi ule uzidi kuwa mzito zaidi kisha akamsogelea taratibu akiwa ameshikilia panga Kali lililofungwa kaniki nyeusi na nyekundu.
Doreen alitamka maneno ambayo aliyajua mwenyewe kisha akamfunua shuka Pamela na kusogeza kisu chake karibu na titi la Pamela. Hakuwa na hofu kama kazi yake haitofanikiwa kwani alikuwa anajiamini na alikiamini kile alichokifanya. Lakini kwa bahati mbaya sana kila alipotaka kumgusa Pamela na upanga ule, Doreen hakuona chochote kitandani pale. Alijaribu tena na tena lakini bado hali ikaendelea kuwa vile vile. Doreen alikasirika sana, akatupa chini upanga ule mlio wake ukamshtua Pamela usingizini.
Doreen alishtuka sana baada ya Pamela kushtuka usingizini, akakimbia haraka na kujibanza kwenye kona moja ya chumba kile kisha akatamka maneno Fulani ya kichawi halafu akatulia kimya.
Pamela aliangaza macho huku na kule chumbani mle lakini hakuona kitu, akainuka kitandani na kuwasha taa kisha akaangalia kila sehemu ya chumba kile lakini hakuona chochote. Akatoka na kwenda msalani, alipokuwa anajisaidia haja ndogo akahisi kuna mtu anamfuata nyuma yake Pamela alishtuka na kuogopa sana kisha akakumbuka jambo muhimu la kufanya kama alivyoambiwa na baba yake. Pamela akasali kwa sauti ya chini na kwa imani kubwa sana kisha akajisaidia na kurudi kitandani, akalala bila kuzima taa.
Doreen alikasirika sana baada ya kumkosa Pamela kwa Mara nyingine. Akaamua kurudi chumbani kwake kupitia kona ile ile aliyokuwa amejibanza.
Doreen alitokea chumbani kwake akiwa na hasira sana. Alijituliza kimya akiwa amekaa chini sakafuni huku akiwa ameshika tunguli na hirizi mkononi mwake. Aliamua kuita mizimu ya kwao ili iweze kumsaidia katika hali ngumu aliyonayo.
Ndani ya sekunde chache alitokea mwanamke mmoja Mzee sana. Kichwa chake kilikuwa kimejaa mvi lakini hakuvaa nguo yoyote isipokuwa kaniki nyeusi aliyovaa kiunoni pamoja na shanga nyingi sana alizokuwa amevaa kiunoni mwake na shingoni. USO wake ulikuwa na makunyanzi mengi sana yaliyokuwa yametawaliwa na vitu kama unga unga mweupe. Alipotua tu chumbani kwa Doreen, nyumba nzima ilitikisika kwani alikuwa ni mtu mkubwa sana katika himaya ya uchawi ya akina Doreen.
"Karibu! Karibu! Mama mtukufu! Mkuu wa wachawi wote! Mwenye nguvu kuliko wote duniani!" Doreen alimkaribisha mgeni wake yule kwa heshima kubwa sana. Yule bibi hakutoa sauti yoyote zaidi ya Kuitikia kwa kichwa tu huku akimsogelea Doreen kwa kutumia makalio yake.
"Doreen! Tangu tumekutuma huku duniani hujawahi kuniita isipokuwa Leo.. Najua una jambo zito linalokusumbua"
"Ndio! Ndio! Mtukufu"
"Sasa inabidi tutoke humu maana si mahali sahihi"
"Sina pingamizi Bi Tatile! Kipenzi cha wachawi wote" yule Bibi alimshika mkono Doreen kisha taratibu kwa kutumia makalio yao wakasogelea kona ya kushoto kwao. Kisha wakatoweka ndani ya jumba lile. Lakini kitandani kwa Doreen waliacha mwili wa Doreen pekee na hata kama angeamshwa kwa kipindi kile basi asingeweza kuamka .
Safari ya wawili wale kwa kutumia usafiri wa ungo huku dereva akiwa Bi Tatile iliwafikisha mpaka eneo la makaburini ambapo walitua na wakaketi hapo kisha wakaendelea na kikao chao kifupi kilichotokea kwa dharula.
"Sema mjukuu wangu.. Mimi ndo Tatile binti Matatila mwenye uwezo wa kubadili nyasi za kijani zikawa nyeupe.."
"Mtukufu lile suala la kupata titi naona linakuwa gumu sana kwangu.. Nimekamilisha kila kitu lakini bado hilo tu.. Tafadhali naomba unisaidie kwa hili..."
"Ha ha ha hah Doreen wewe una uwezo mkubwa sana wa kukamilisha hilo.. Unaweza ukafanya hivyo haraka sana ila kuna jambo moja tu! Unatakiwa ufanye."
"Jambo gani mtukufu? Niambie tu maana nimechoka kuhangaika" alisema Doreen. ****
Majira ya saa kumi na moja jioni Dada wa Mama Eddy aliwasili nyumbani kwa Mr Aloyce. Alipokelewa vizuri sana na Bwana Aloyce pamoja na Eddy lakini ilikuwa tofauti sana kwa mama Eddy kwani alimkaribisha Dada yake kama vile alimkaribisha adui yake ndani ya nyumba. Suala hilo liliibua maswali mengi sana kwa Mr Aloyce pamoja na mgeni wao.
"Mama Eddy.. Nakuomba chumbani Mara moja..." Alisema Baba Eddy kisha akaingia chumbani. Mama Eddy alimfuata mumewe ili amsikilize kile anachotaka kumweleza.
"Mke wangu... Mbona unaniabisha kwa shemeji yangu?"
"Kivipi?"
"Dada yako amekuja lakini unamsalimia kama hutaki vile.. kwanini?" Aliuliza baba Eddy kwa mshangao.
"Nimejisikia tu.."
"Hapana mke wangu usiwe hivyo... Nakuomba basi onesha kumjali mgeni tena nduguyo wa damu.."
"Siwezi kumjali mchawi mkubwa yule..." Alisema mama Eddy akiwa anajishumburua midomo yake kwa dharau.
"Unasemaje? Dada yako mchawi kivipi?"
"Amemroga mwanangu..."
"Umejuaje au nawewe mchawi? Maana haiwezekani umtuhumu mwenzio mchawi wakati huna uhakika?" Alisema Baba Eddy kwa hamaki. Hakutaka kuamini kile alichokisa mkewe.
"Leo hii unaniambia mimi mchawi? OK sawa... " alisema Mama Eddy na kwenda sebuleni kwa hasira.
Alisimama wima akiwa ameshika mkono kiunoni huku akimtazama dada yake kwa dharau.
Dada yake alipigwa na butwaa sana, alibaki anamshangaa mdogo wake kwa vitendo vya dharau anavyomfanyia.
"Wewe!" Alisema Mama Eddy.
"Naomba utoke kwenye nyumba yangu.. Ulichomfanyia Eddy kinatosha..."
"Mimi?"
"Kumbe naongea na nani kama sio wewe mpumbavu..." Alisema Mama Eddy akidhihirisha chuki kubwa aliyonayo moyoni mwake. Eddy alimtazama mama yake kwa mshangao sana akiwa haelewi sababu ya mama yake kumfanyia unyama ule dada yake wa damu. Hakuna aliyefahamu ukweli kuwa yule hakuwa mama Eddy halisi.
"Mama... Mama mkubwa amekosa nini?"
"Hebu kelele huko na wewe.. Hujui kama huyu ndo aliyekuroga?"
"Sio huyu mama..." Eddy alimtetea.
"Hebu ondoka hapa.. Kwanza hayakuhusu.." Alifoka Mama Eddy.
"Sasa na mimi naondoka na mamkubwa.. Sibaki hapa?" Alisema Eddy.
Wakati huo Mr Aloyce alifika sebuleni pale na kuanza kumuomba msamaha mgeni yule asiye na hatia....
ITAENDELEA.....
Usikose
Subscribe to:
Posts (Atom)