About KABENDE.COM

Manual Description Here: Ea eam labores imperdiet, apeirian democritum ei nam, doming neglegentur ad vis.

RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 30

Riwaya:A  WIZARD STUDENT (MWANAFUNZI MCHAWI)
Mtunzi:ENEA FAIDY

SEHEMU YA 30

....Dorice aliendelea  Julia huku matone yake ya machozi yakiwa damu. Ghafla akajikuta ana uwezo wa ajabu ambao hajawahi kuufikiria kuwa nao hata siku moja. Alijibadilisha sura na kuwa kiumbe wa kutisha, macho yalikuwa kama ya paka, uso wake ukawa mweusi tii kama mkaa, kucha zake zikawa ndefu sana na meno yake mawili yalichomoza nje ya kinywa chake. Mansoor alicheka kicheko kikali cha kutisha huku sauti ya kicheko chake ikiambatana na mwangwi. Radio zikapiga mfululizo Dorice akatoweka ghafla na kumuacha Mansoor.  
Pete aliyokuwa amevalishwa Dorice ilimpa uwezo mkubwa na wa ajabu. Alipata uwezo wa kupotea na kujibadilisha kadri atakavyo lakini sharti kubwa alilotakiwa kufanya ilikuwa ni lazima urudi tena kwa Mansoor baada tu ya kumaliza kazi yake inayompeleka duniani.

Dorice alikuwa ametokeza katika eneo lenye Giza Giza lilitowaliwa sauti za wadudu. Palikuwa na utulivu mkubwa sana , kwani eneo lile halikukaliwa na mtu yeyote zaidi ya ndege, wadudu na wanyama wadogo wadogo. Dorice alibaki anajishangaa, alijiuliza amefika vipi eneo lile akiwa peke yake bila Mansoor.
"Ina maana nimekuwa na nguvu za kijini?" Alijiuliza  Dorice. Ghafla upepo mkali ukapuliza eneo lile, Dorice alitazama huku na kule ili kujua nani alikuwa mgeni wake kwa wakati ule. Ghafla Mansoor akajitokeza akiwa anacheka kicheko cha kutisha sana kisha akapiga hatua za taratibu kumsogelea Dorice.
"Kwanini umefika huku?" Aliuliza Mansoor kwa ghadhabu.
"Sijui nimefikaje" alijibu Dorice.
"Muda wako wa kuondoka kwenye himaya yangu bado Dorice, nilikuwa na jaribu kukupa ladha ya vile utakavyokuwa baada ya wakati kutimia"  alisema Mansoor.
"Kwahiyo unataka nirudi?"
"Ndio.. Tunarudi wote"
"Hapana Mansoor sitaki kurudi tena Kule" alisema Dorice.
"Ni lazima urudi maana bado sijakupa maelekezo"
"Hayo maelekezo nipe hapa hapa"
"Haraka haraka ilimfanya chura apate ngozi ya mabaka" 
"Hata hivyo siwezi kurudi"

Yalizuka mabishano makali baina ya Dorice na Mansoor kwani Dorice hakutaka kurudi kwenye himaya ya Mansoor tena. Alitaka aachwe huru na arudi kwao, lakini mkongwe ni mkongwe tu licha ya mabishano Yale Mansoor aliibuks mshindi baada ya kumchukua Dorice kinguvu kwa kutumia uwezo mkubwa wa kijini alionao. Katika eneo walilokuwepo ukatokea upepo mkali na kuwavuta wote wawili kisha ndani ya muda mfupi wwlijikuta wametokea katika himaya ya akina Mansoor.  Dorice alikasirika sana.

*****
"Mama mbona sikuelewi" aliuliza mlinzi kwa hofu huku akimtazama Mama Eddy kwa woga.
"Wewe!" Alisema mama Eddy akiwa amevimba kama mbogo huku akimsonta mlinzi yule kwa kidole chake na kumfanya mlinzi yule atawaliwe na hali ya sintofahamu.
"Nimefanya nini mama?"
"Kaa mbali na Eddy... Nakusisitiza Tena kaa mbali na Eddy la sivyo utakiona cha mtema kuni paka shume we we!"alisema Mama Eddy huku akipiga hatua na kutaka kuondoka.
Alitembea kwa hatua chache tu kisha akamgeukia tena mlinzi na kumuonya vikali kuwa asiwe karibu na Eddy. Mlinzi yule hakuelewa mwanamke yule ana maana gani kumwambia vile. Alibaki na maswali mengi kichwani mwake huku  akimsindikiza kwa macho mwanamke yule aliyejongea taratibu machoni mwake baada ya kuingia ndani ya jumba la kifahari la  Mr Alloyce. Mlinzi aliachana na mwanamke yule kisha akaendelea na kazi zake za kupunguza maua.

Mama Eddy aliingia ndani na kumkuta Mr Aloyce akiwa ameketi kwenye sofa huku USO wake ukidhihirisha furaha kubwa aliyonayo moyoni mwake. Alifurahia sana kurudi kwa mkewe katika familia yao ili waendelee kuijenga na kuidumisha furaha yao ikiwa ni pamoja na kutafuta tiba ya tatizo la mtoto wao wa pekee.
"Mwanangu yuko wapi?"  Aliuliza Mama Eddy huku akitabasamu. Baba Eddy alinyanyua kichwa chake na kupaza sauti yake akimwita mwanaye. Bila kuchelewa Eddy alirudi sebuleni na kumkumbatia mwanamke yule aliyedhani ni mama yake. 
"Mama bora umerudi.. Tulikuwa wapweke sana humu ndani!" Alisema Eddy na kumfanya mwanamke yule atabasamu kwa furaha. 
"Nimerudi mwanangu" alisema mwanamke yule. Familia ile ikarejewa na furaha iliyokuwa imepotea ndani ya muda mfupi uliopita.
Wakiwa wameketi sebuleni pale kwa utulivu wa hali ya juu, ghafla simu ya Mr Aloyce iliita, akaitoa mfukoni na kuangalia nani alimpigia. Alipotazama tu akaona namba aliyoisevu "Shem Dar" akashtuka kidogo kisha akapokea.
"Ndio..ndio shemeji!" Alisema.
"Nipo njiani na sio muda nafika hapo nyumbani" ilisikika sauti ya Dada yake Mama Eddy.
"Unakuja hapa kwangu?"
"Ndio.. Si ulisema kuna matatizo!"
"Mh Haya karibu"
Baada ya mazungumzo hayo simu ikakatika ndipo Mr Aloyce akaona si vyema kumfichs mkewe kuhusu jambo lile. Akamweleza kila kitu kuhusu chanzo cha Dada yake kufika nyumbani kwao.
"Ulimwambia kuna tatizo gani?" Alisema mama Eddy kwa mshangao.
"Nilimwambia tu kuna tatizo na sikumweleza ni tatizo gani. "
"Vizuri! Akija hapa usimweleze chochote kuhusu suala la Eddy" alisema Mama Eddy. Kauli hiyo ilimshtua Mr Aloyce kwani hakuona haja ya kumficha shemeji yake kuhusu jambo lile.
"Kwanini nisimwambie? Hujui kama anaweza kutusaidia.. Pengine hata kwa ushauri..." Alisema Baba Eddy.
"Nimesema usimwambie chochote.." Alisema Mama Eddy na kuinuka kitini kisha akaondoka sebuleni pale na kuwaacha Mr Aloyce na Eddy.
Mr Aloyce alibaki na mshangao sana kwani alikumbuka jinsi ambavyo Mama Eddy wanavyopatana na kuelewana kama mapacha iweje Leo amfiche matatizo yake?. Alishindwa kuelewa sababu akabaki kimya kitini pale. 

****
 Mama Pamela na mwanaye waliendelea kuusubiri usingizi uwachukue ili kupambazuke haraka. Usingizi ulichelewa sana kuwachukua lakini haukuwaacha kabisa. Baada ya kuusubiri kwa muda mrefu wakiwa na hofu kupita kiasi hatimaye usingizi ukawapitia. Kila mmoja alilala fofofo kutokana na uchovu pamoja na mihangaiko mingi iliyosababishwa na mauzauza ya usiku ule.
Hatimaye kukapambazuka lakini bado wanafamilia ile walikuwa wapo katikati ya usingizi. Mlango wa chumba iligongwa na kumfanya mama Pamela ashtuke usingizini na kusikiliza nani aligonga.
"Mama" sauti nyororo ya Doreen ilipenya masikioni mwa Mama Pamela ikiwa na wingi wa adabu na upole uliokithiri. Bila kusita mama Pamela Aliitikia wito na kumsikiliza Doreen anahitaji nini.
"Hauendi kazini? Pia Dada Pamela haendi shule?" Aliulizs Doreen.
"Hatuendi... Wote tupo likizo.." Alijibu Mama Pamela .
"Sawa mama.. Nilifikiri mmesahau.. Ngoja niendelee na kazi"
"Hebu njoo kwanza.." Mama Pamela alimwita Doreen na kutaka aingie chumbani.
"Abee mama" Doreen aliitika kwa heshima na kusogelea karibu kabisa na kitanda cha Mama Pamela.
"Hivi usiku ulilala salama?"
"Ndio kwani vipi?" Aliuliza Doreen kwa mshangao.
"Mh! Kweli?"
"Ndio.. Kwani nini kilitokea"
"Duh basi kama ulikuwa salama sawa... Hakuna tatizo!" Alisema mama Pamela.
Doreen alijifanya kushangaa kupita kiasi, lakini hakuuliza zaidi. Aliachana nao na kwenda jikoni kuandaa chai.

Alichemsha maji na kuweka majani ya chai. Na baada ya kuhakikishs imechemka vizuri akaiipua vizuri kisha akatemea mate halafu akaiweka kwenye chupa ya chai huku akicheka.
"Mtakoma mwaka huu..." Alijisemea Doreen kisha akapeleka chai mezani. Akarudi jikoni na kuchemsha maini ya ng'ombe lakini alipokuwa akichemsha maini yale  alichanganya na maji Fulani yaliyokuwa kwenye kichupa Fulani kidogo.
"Na mtakula sana uchafu wangu... Huu mkojo tu! Bado vingine vinakuja" alisema Doreen kwa sauti ya chini.
Maini  Yale yalichemka vizuri na kutoa harufu ya kuvutia sana. Baada ya kuyaivisha vizuri akachukua mayai ns kuyakaanga vizuri kisha akapeleka mezani na kuandaa vizuri.
Majira ya saa tatu asubuhi Mama Pamela na mwanaye waliamka. Wakaoga na kwenda chumba cha Julia chakula.
"Doreen kumbe umesha andaa kila kitu" alishangaa Mama Pamela.
"Ndio mama! Karibuni"  Aliitikia Doreen.
"Asante.." Alisema mama Doreen huku akiketi na kusogeza karibu mikate, akaipaka blueband.
"Mbona wewe huji kula?" Alimuuliza Doreen.
"Mimi tayari.. Hivyo ni kwaajili yako na dada Pamela"
"Oh sawa.. Mwite Dada yako aje kula maana ni mvivu kweli" alisema mama Pamela huku akianza kukishughulikia chakula kile.  Punde tu Pamela naye akaenda mezani pale na kuanza kula.

Wakati huo Doreen alikuwa pembeni yao akiwatazama jinsi wanavyokula chakula kile kichafu. Aliwasikitikia sana moyoni mwake lakini wao walimmwagia sifa tele kwa utamu wa chakula kile. Kila mmoja alimsifu Doreen kwa kumwambia ni fundi wa Mapishi.

"Doreen mwanangu.. Nataka nikuulize kitu" alisema Mama Pamela huku akimeza funda moja la chai ns kutua kikombe taratibu kwenye meza nzuri na safi ya kioo. Kauli ile ilimshtua kidogo Doreen na kumfanya amuulize vizuri mama Pamela.
"Kitu gani mama?" 

............
.............
..............
..............
ITAENDELEA.......
LIKE, COMMENT, SHARE..

MPAKA HAPO ILIPOFIKIA.. JE UMEJIFUNZA NINI KWENYE HADITHI HII? 
TIRIRIKA...
Read More...

RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 29

RIWAYA:A WIZARD STUDENT (MWANAFUNZI MCHAWI)
MTUNZI:ENEA FAIDY

SEHEMU YA 29

.....MR Aloyce alizidi kumkazia macho mkewe akahisi ni mrembo zaidi ya Mama Eddy yule anayemfahamu yeye. Halafu alikuwa na madaha sana kuzidi vile alivyomzoea. Wasiwasi ukamtanda akilini make na kumfanya asimwamini sana mwanamke yule kuwa ndiye mkewe halisi.
"Mbona unaniangalia sana? Umemisi busu langu nini?" Aliuliza Mama Eddy.
"Hapana wala usijali"
"Ok kama wewe hukumiss basi Mimi nilimisi sana kiss lako mpenzi"
Alisema Mama Eddy huku akimsogelea Mr Aloyce kwa ukaribu zaidi na kumshikashika kidevu kwa mahaba. Mr Aloyce alionesha kutojali mguso ule aliopapaswa na mikono laini ya mkewe. Hakuelewa ni sababu zipi zilizomfanya asimjali mwanamke yule kwa kiasi kile ila moyo wake ulikuwa mzito sana.
"Baby mbona hivyo...? Embu usiwashe gari kwanza mpaka unibusu" alisema Mama Eddy kwa sauti iliyojaa mdeko wa kimahaba. Mr Aloyce hakutaka kukiri udhaifu, akaachia usukani na kusogeza mdomo wake karibu na mdomo wa mkewe kisha akambusu.
 Busu lile lilimpa nafasi nzuri sana Mama Eddy ya kupenyezapenyeza mpaka kuingiza ulimi wake mdomoni kwa Mr Aloyce. Kisha wakabadilishana mate yao kwa mahaba. Lakini wakati tendon hilo likiendelea, Mwanamke yule alimwachia vitu Fulani Mr Aloyce bila yeye mwenyewe kujua. Na ilikuwa ni dawa Kali ya kumfanya Mr Aloyce amwamini mwanamke yule kuwa ndiye mkewe halisi wakati hakuwa yeye. Alikuwa ni mwanamke kutoka himaya ya akina Doreen na alitumwa nyumbani kwa Mr Aloyce ili afanye kazi muhimu sana aliyotumwa. 

Kwa vile alivyomfanyia Mr Aloyce, alifanikiwa kuziteka akili za Mwanaume yule. Baada tu ya busu lile la huba, Mr Aloyce alijkuta akimpenda sana mwanamke yule akijua ndie Mkewe halisi na kumbe haikuwa hivyo. Wasiwasi wake ulifutika kichwani mwake,  pendo la dhati likatawala moyoni mwake. 
"Tuondoke mume wangu" alisema mama Eddy kwa sauti ya upole iliyojaa huba huku akiwa ameachia tabasamu pana usoni mwake.
"Usijali mke wangu.. Nilikukumbuka sana... Nina imani hata mwanetu anakusubiri kwa hamu sana." Alisema Mr Aloyce huku akishikilia vizuri usukanu na kuondoa gari kwa kasi sana.

Mr Aloyce aliendesha gari kwa kasi ya ajabu na baada ya masaa machache tu waliwasili eneo la Ipogoro Iringa kisha wakaelekea nyumbani kwao. 
Walifika getini wakapiga honi geti lilifunguliwa. 
Mr Aloyce aliegesha gari pembeni kisha akashuka kwa furaha kubwa, na baada ya hapo akaelekea upande wa pili wa gari yake na kumfungulia mkewe huku tabasamu mwanana likiwa limechanua mdomoni mwake.
"Shuka malkia wangu... Tumeshafika kwetu.." Alisema Mr Aloyce huku mwanamke yule anayefanana kwa kila kitu na Mama Eddy akishuka kwa madaha kisha akamkumbatia Mr Aloyce na kumbusu. Wakati yote hayo yakiendelea Mlinzi alikuwa pembeni yao akishuhudia penzi la zamani lililochipua upya tena kwa kasi ya ajabu.
"Mh bosi naona mama Amerejea.." Alisema mlinzi kimzaha.
"Ndio.."alijibu Mr Aloyce kwa furaha.
"Baby nataka kuongea jambo na mlinzi wetu naomba utuache kidogo.." Alisema Mama Eddy.
"Ok ila kuwa makini tu nisije kupinduliwa na houseboy.." Alisema Mr Aloyce na kuondoka zake huku akimsisitiza mkewe asichelewe.
Baada ya Mr Aloyce kuondoka pale, Mwanamke yule alimsogelea mlinzi na kumtazama kwa ghadhabu Kali. Hali hiyo ilimtisha sana mlinzi na kumfanya ajiulize maswali mengi ambayo alishindwa kujijibu mwenyewe.

****
Mama Pamela aliishiwa nguvu kabisa. Alijiuliza sana ni kwanini mwanaye amelala chooni kule ilhali ana kitanda kizuri cha kumfaa? Maswali yake hayakuwa na majibu akajikuta anaishia kupiga makofi kwa mshangao.
"Pamela!" Alimwamsha mwanae ambaye bado alionekana ana usingizi mzito sana. Alimtikisa tikisa mpaka alipofanikiwa kumwamsha kabisa. Pamela aliinuka, lakini alibaki mdomo wazi baada kuona mazingira aliyopo si ya kitandani kwake.
"Mama nipo wapi hapa? Mbona kama chooni?" Aliuliza Pamela kwa mshangao.
"Nikuulize wewe mwanangu.. Umefikafikafikaje mpaka ukalala chooni?" Aliuliza Mama Pamela.
"Mbona sielewi mama" alisema Pamela.
"Haya chukua hilo shuka lako twende chumbani.. Hayo mengine tutajua huko huko.." 
Walitoka chooni mle na kuelekea chumbani kwa mama Pamela. Pamela alitoa nguo aliyokuwa amevaa kwaajili ya kulalia kisha akavaa nyingine kwani ile tayari ilishapata unyevunyevu wa chooni.
"Lakini mama mbona Doreen hatujaenda kumwangalia si atahisi tunamtenga.." Alisema Pamela.
"Ila kweli"
"Tumfate basi.." Alisema Pamela kisha wakainuka na kwenda chumbani kwa Doreen. Kulikuwa na Giza totoro ambalo bila msaada wa tochi basi wasingeona chochote. Walimulika kitandani kwa Doreen na kumwona Doreen akiwa amelala fofofo. Walimsogelea kwa ukaribu na kumwamsha lakini Doreen hakuitikia. Pamela na mama yake walitazamana mshangao.
"Mbona haamki?" Walinong'ona taratibu.
"Isije ikawa ndo amek.. Amepata matatizo mengine" alisema Pamela.
"Doreen! Doreen" Mama Pamela aliita kwa sauti kubwa lakini Doreen bado hakuamka.
"Tumuache basi tutamkuta kesho yawezekana mwenzetu hajakumbwa na mauzauza" alisema Pamela kisha wakarudi chumbani kwa Mama Pamela kupumzika kidogo maana Pamela asingeweza kulala peke yake kutokans na woga aliokuwa nao kwa usiku ule.

***** 

"Umeshika nini hicho Mansoor" aliuliza Dorice kwa woga .
"Nimeshika Pete" alijibu Mansoor. Jibu hilo lilimshangaza Dorice kwani alichokiona mkononi kwa Mansoor haikuwa Pete Bali alikuwa nyoka mkubwa aliyejiviringisha kama Duara kiganjani kwa Mansoor. 
"Pete gani hiyo?" Dorice alizidi kuogopa.
"Ni pete ya kukupa wewe ili uwe na nguvu ya kurudi duniani na kufanya lolote utakalo..." 
"Mbona namuona Nyoka?"
"Fumba macho kisha ufumbue nikikuruhusu" alisema Mansoor kisha Dorice alifanya kama alivyoambiwa. 
Mansoor alisogeza mkono wa Dorice kisha akchuku kidole Chanda na kumwambia  Dorice afumbue macho yake.
Dorice alifumbua macho yake na kutazama kidole chake. Alishtuka kuona pete inayong'aa sana kidoleni mwake.
"Umenivisha SAA ngapi?" 
"Nimekuvisha ulipofumba macho" 
"Mbona sikuhisi chochote? Na je yule nyoka yuko wapi?"
"Sikushika nyoka.. Nilishika pete"  alisema Mansoor.
Ghafla Dorice alijiona wa tofauti sana.  Kichwa kikaanza kumgonga kwa kasi sana, akaanza kulalamika. Na kadri alivyolalamika ndivyo kadri maumivu yalivyomzidia.
Machozi yalianza kuchuruzika lakini cha ajabu, matone ya machozi yake hayakuwa ya kawaida kwani kila tone alilodondosha lilikuwa damu. Dorice alijishangaa sana lakini Mansoor akaangua kicheko kikali kilichomshangaza Dorice.

........................................…...............................................................................

ITAENDELEA.
LIKE, COMMENT, SHARE
Read More...

RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 28

Riwaya:A WIZARD STUDENT (MWANAFUNZI MCHAWI)

Mtunzi: ENEA FAIDY

SEHEMU YA 28

.... Leyla alikuwa amechanganyikiwa sana baada ya mumewe kuwa katika Hali ile. Alishindwa kuelewa atafanyaje ili kujimudu katika familia yake kwani Mwalimu John ambaye ni mumewe asingeweza kurudi tena kazini. Kilichomfanya anyong'onyee zaidi ni hali ya Judith kwani hakuweza kuongea wala kusikia. Leyla alikosa raha sana, akakaa kitini akiwa na mawazo mengi sana. Alijiuliza afanye nini ili aweze kuwaokoa wahanga wa tatizo asilojua limetona na nini. Akiwa katika kutafakari hayo yote ghafla wazo muhimu lilimjia kichwani mwake. Leyla alichukua simu yake na kutafutw namba fulani kisha akapiga. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa kisha ikakakata. Leyla hakukata tamaa akapiga tena lakini majibu yakabaki Yale Yale, simu haikupokelewa akajaribu tena na tens simu ikapokelewa.
"Bwana asifiwe mchungaji.." Alizungumza Leyla kwa sauti ya unyenyekevu sana kwani aliyempigia alikuwa ni mchungaji wake.
"Amen.. Unasemaje?" Alijibu mchungaji yule kama vile hataki kuzungumza.
"Samahani mchungaji nina shida... Naomba msaada wako!" Alisema Leyla.
"Shida gani"
"Kuhusu familia yangu!"
"Kama ni mumeo mama... Chukua imani hapo ulipo anza maombi Mimi sina muda... Nina mambo mengi ya kufanya.." Alisema mchungaji yule kwa ukali kiasi jambo lililomtisha sana Leyla kwani hakutegemea kama mchungaji wake angemjibu vile. 
"Pastor! Tafadhali nisaidie.." Leyla alimbembeleza mchungaji lakini hakumuelewa. Na mchungaji huyu ndiye aliyefanya mazishi ya mwalimu John.
"Kwasasa sipo nyumbani.. Nipo mbali kikazi..." Alisema Mchungaji yule. Kiukweli ilikuwa vigumu kwa Leyla kuamini maneno ya mchungaji wake kwani Sikh zote aliamini mchungaji wake angekuwa ndiye mfariji lakini haikuwa hivyo.
"Cha kukusaidia labda nitawata wanamaombi waje kukusaidia" alisema mchungaji na kukata simu. Leyla alishindwa afanye nini kwani hats ndugu zake walimtenga. Ilipita nusu SAA nzima , mlango wake ukagongwa. Alifurahi sana kwani alijua tayari mchungaji amewasiliana na wanamaombi ili waje kuombea familia yake. Alinyanyuka kitini na kwenda moja kwa moja kufungua mlango.

***

Mama Pamela alizidi kutetemeka kwa woga sana, alijikunyata kama mgonjwa kitandani kwake. Lakini alizidi kuisikia sauti ya mwanae ikiendelea kumwita. Mama Pamela akazidi kupata hofu, japo aliogopa sana lakini aliamua kuinuka kitandani na kunyata taratibu kuelekea chumbani kwa Pamela. Na hii ni kwa sababu damu nzito kuliko maji .

Nyumba ilitawaliwa na kiza kizito sana, hivyo ilimpa shida sana Mama Pamela kuelekea chumbani kwa mwanae. 
Aliingia chumbani kwa Pamela na kuita taratibu "Pamela! Pamela!" Lakini Pamela hakuitikia. Mama Pamela alisogelea kitanda cha Pamela na kuanza kupapasa papasa lakini cha ajabu hakuona dalili zozote za uwepo wa mtu kitandani pale. Mama Pamela alizidi kuchanganyikiwa sana. Akaita tena "Pamela! Pamela!" Lakini bado hakukuwa na sauti yoyote iliyoitikia. Mama Pamela alihisi akili yake inavurugika. Akauvua woga wake na kumuita Pamela kwa sauti kubwa lakini bado hakuitikia. 
Mama Pamela alirudi chumbanu kwake na kupapada sehemu ilipokuwepo simu yake na baada ya kuipata alimshukuru Mungu. Kisha akawasha tochi na kuanza kumulika kila chumba. 
Aliingia chumba cha kwanza akamulika lakini hakuona MTU, akamulika, cha pili, cha tatu na kisha akaingia jikoni lakini bado hakumuona Pamela. Roho ya Mama Pamela iliingiwa simanzi, akajua mwanaye amepotea kwa mazingira ya kutatanisha . akaingia bafuni na kumulika lakini Hakumkuta Pamela. Mama Pamela alizidi kuchanganyikiwa zaidi.
"We Mungu bora wangenichukua Mimi sio mwanangu Pamela," alisema Mama Pamela akiingia chooni. 
Mama Pamela alistaajabu sana alichokutana nacho. Alimkuta Pamela akiwa amelala chooni huku kajifunika blanketi lake vizuri."

"Pamelaa!" Aliita mama Pamela kwa mshangao na mpaka wakati huo mama Pamela hakujua Doreen anaendeleaje.

****
Mr Alloyce alibaki njia panda, alikuwa haelewi cha kufanya juu ya mwanamke yule. Alijiuliza amkubalie kama mkewe au asimwamini? Mawazo yake hayo mawili yalimezwa na ukarimu wa mwanamke yule kwa jinsi alivyoonesha kumjali Mr Aloyce.
"Mime wangu... Mbona hunichangamkii? Baba Eddy jamani" alisema mwanamke yule na kumsogelea Mr Aloyce "hivi kweli we ni Mke wangu? Mama Eddy?" Aliuliza Mr Alloyce kwa wasiwasi.
"Kha! Kumbe huniamini mume wangu?" Alisema 
"Mbona ulitokea kama Chatu?"
"Hahahah unatakiwa kuniamini mume wangu!" Alisema mwanake yule na kumsogelea Baba Eddy kisha akamkumbatia.
Mr Aloyce alitamani kumwamini mwanamke yule kama ndo mkewe lakini moyo wake ulisita. Alimsogelea na kumkumbatia lakini moyoni make alikuwa na mashaka sana.
"Nakupenda mime wangu.. Naomba tuwahi nyumbani ili nikamwone mwanangu" alisema mama Eddy.
"Sawa" alisema Baba Eddy huku akifungua mlango wa gari.
"Lakini unanishangaza mume wangu?"
"Nakushangaza na nini?"
"Huna amani moyoni mwako.. Kwanini?"
"Usijali Niko sawa..." 
Wallingia kwenye gari kisha Mr Aloyce aliwasha gari na kuanza kuendesha. Aligeuka kumtazama mkewe yule aliyekuwa ameketi pembeni yake, lakini kuna kitu kilimshangaza..

ITAENDELEA..
LIKE,COMMENT, SHARE

Read More...

Serikali Yatangaza Mwongozo Mpya wa Elimu Kuwa Masomo ya Sayansi ni Lazima Yasomwe Na Wanafunzi Wote

SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. 

Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Tanga  na Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na mamia ya walimu wa elimu ya msingi kwenye mafunzo ya muda mfupi kuhusu mtaala mpya wa kufundishia wanafunzi wa darasa la tatu na nne.

Alisema hivi sasa nchi imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa kati ambao ni wa viwanda, hivyo suala la sayansi haliwezi kuepukwa kwa sababu ni wakati sasa wa kuwa na wataalamu wengi wa fani za sayansi watakaoweza kutosheleza mahitaji ya sekta ya viwanda nchini.

Alisema kutokana na uhaba wa wataalamu wa sayansi nchini kwenye maeneo mengi, wizara imeamua kuanzia sasa wanafunzi wote wa elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, watalazimika kusoma masomo ya sayansi na kufanya mtihani wa masomo hayo, na kwamba baada ya matokeo kutoka ndipo watafanya uamuzi ama wa kuendelea nayo au la.

Hatua hii kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, itamlazimisha mwanafunzi kusoma kwa bidii ili kuhakikisha anafaulu masomo hayo ingawa hivi sasa wanafunzi walio wengi wanadai masomo hayo ni magumu, ndiyo maana wanachagua kusoma masomo ya sanaa.

Alisema ili kuhakikisha azma ya serikali ya wanafunzi wanapata vitendea kazi vya masomo hayo, Sh bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwenye shule zote za sekondari nchini ili kuwepo na zana za kufundishia kwa ajili ya masomo ya sayansi.

"Mafunzo ya vitendo sasa sio mbadala ni lazima, na yatafanywa kama sehemu ya masomo na wanafunzi wote watalazimika kuyafanya kwa vitendo ili wawe na uelewa wa walichosoma kwa manufaa ya taifa,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuona kiwango cha elimu kinachotolewa nchini kina hadhi sawa na elimu itolewayo na mataifa mengine ili kupata wataalamu wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya soko hata kama sio wote wataajiriwa ila hata wale wasiopata ajira wajiajiri kupitia elimu waliyopata.

Aliwataka walimu waliohudhuria mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia uwezo wao na elimu waliyopata kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya taaluma ya ualimu ili kuwajengea msingi mzuri wa elimu wanafunzi wa shule za msingi.

Akizungumzia kauli ya Profesa Ndalichako, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAMANGOSCO), Mahmoud Mringo alisema ni uamuzi mzuri ila umekuja kwa kuchelewa kwa sababu mahitaji ya wataalamu wa sayansi nchini ni makubwa kuliko idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo.

Alisema pamoja na uamuzi huo mzuri uliochukuliwa na serikali, lakini bado kutakuwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo, maabara na maktaba na kwamba hali hiyo inaweza kusababisha mahitaji ya walimu hao kutoka nje yakaongezeka.

Katibu wa Tamangosco, Benjamin Mkonya alisema ni hatua nzuri ingawa utekelezaji wake utakuwa na changamoto nyingi kwa sababu hali halisi ya mazingira ilivyo nchini.

Alisema ikiwa serikali inadhamiria kutekeleza azma hiyo ni vyema kipengele cha vigezo vya shule kuwepo ambavyo vimeainishwa ndani ya sheria ya elimu nchini, vikaangaliwa ambavyo ni uwepo wa maabara ya kutosha, maktaba yenye vifaa na walimu wa kutosha.

Alisema iwapo vigezo hivyo vikiangaliwa shule ambazo hazijakidhi vigezo hivyo zikafutwa na vifaa vilivyopo kwenye maabara na maktaba hizo zikaongezwa kwenye shule zenye vifaa hivyo ili kusaidia utekelezaji wa azma hiyo ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Walimu washiriki wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo ambayo walisema ni mazuri na yameongeza kiwango chao cha uelewa na kuwaongezea mbinu za ufundishaji sambamba na kukuza morali ya kazi zao.

Pamoja na kushukuru, wameomba wizara hiyo iangalie jinsi ya kuweka posho kwa baadhi ya maeneo ya kazi, hususan kwenye vituo vya kazi vilivyopo pembezoni na kwenye mazingira magumu ili kuwajengea walimu motisha wa kufundisha maeneo hayo.

Walimu waliohudhuria mafunzo hayo ni 480 wanaotoka halmashauri za Bumbuli, Mji wa Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Read More...