RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA SITA

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Sita
Mtunzi:  Enea Faidy

IIlipoishia sehemu ya  Tano ( kama hukuisoma BOFYA HAPA ).

Eddy alimwacha Dorice Solemba, akilia na moyo nje ya darasa. Na alipoingia darasani Eddy alifuatwa na Doreen kwenye kiti chake, na alitaka kumwambia kitu muhimu....

Endelea...
Doreen alizidi kujilegeza sana kwa Eddy ili amteke kimawazo na kiakili sawasawa. Alirembua macho kama aliyekula kungu huku akimtazama Eddy.. Hakika kwa urembo aliokuwa nao Doreen na vituko alivofanya alizidi kuziteka hisia za Eddy haswa. 

Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.

"Eddy!" Doreen aliita kwa sauti ya mvuto sana.
"Naam"
"niambie basi.."
"ah!.. Doreen kama nilivosema awali wewe in mzuri sana hivyo basi .... nataka uwe mpenzi wangu.. please! naomba unielewe!" Eddy aliongea kwa sauti ya chini ili majirani wasiweze kusikia.
"Eddy! we ni shemeji yangu siwezi kumsaliti rafiki yangu Dorice!" Doreen alijifanya kukataa ingawa moyoni mwake alifurahia ushindi wa kumpata Eddy ilhali warembo wore shuleni pale waliikosa nafasi ile isipokuwa Dorice.
"Doreen! plz naomba nikubalie nakupenda sana "
"Na Dorice je?"
"habari za Dorice achana nazo me nimeachana nae, nakupenda wewe"
"mi sitaki Eddy!" sauti aliyoitoa Doreen ilionesha kabisa alikuwa anataka Ila alivunga tu.
"Nikubalie Dori.. nakupenda Doreen.. usinitese!" Eddy alisema huku machozi yakimlengalenga kwani hakutaka kumkosa Doreen. Ama kweli dawa za Doreen alizotafuna kabla ya kumfuata Eddy zilifanya kazi vizuri sana.
"Okey! nakubali kuwa na wewe!"
"Oh my God kweli Doreen unanipenda? asante sana!" Eddy aliachia tabasamu mwanana na alitamani hata kumkumbatia Ila aliogopa kufanya vile kwani walikuwa darasani.
"Nakupenda Eddy Ila kuna sharti moja muhimu inabidi ufate ili uwe na Mimi..."
"sharti gani tena?" Eddy alishtuka
"upo tayari?"
"ehm.. ah ndio coz I love u.. ntafanya"
"good.. nafurahi sana"
"Niambie basi mpenzi.." alisema Eddy akitabasamu.
"usijali nitakuambia baadae..."
Alisema Doreen huku akiinuka kitini na kuondoka zake. Eddy alikuwa na furaha sana hakuweza hata kusoma zaidi ya kumfikiria Doreen na kila Mara aliachia tabasamu.

Ilikuwa ni mchana majira ya SAA nane na nusu ambapo kengele iligongwa katika shule ya sekondari Mabango ambapo iliwaataarifu wanafunzi wote kuwa muda wa vipindi umekwisha na ni muda wa kupata chakula cha mchana.

Lakini haikuwa hivyo kwani wanafunzi walitakiwa waende mstarini ambapo Habari za kusikitisha sana zilipenya mioyoni mwa wanafunzi wote wa shule ile.

"Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi ameaga dunia Leo asubuhi kwa kifo cha ghafla kilichompata ofisini kwake..pia walimu wawili wana hali mbaya na wamefikishwa hospitalini kwa matibabu!" ilikuwa sauti ya masikitiko sana kutoka kwa Mwalimu Gallus iliyoonesha simanzi nzito sana aliyokuwa nayo.

Mwalimu huyo alishusha pumzi ndefu sana na kuendelea " Maombi yenu in muhimu sana kwa walimu wenu ambao wapo hospitali... na..." mwalimu Gallus alishindwa kuendelea kuzungumza kwani machozi yalikosa adabu yakashuka kwa kasi hivyo akaamua kuondoka eneo lile.

Wanafunzi wote waliondoka lakini mwishoni alibaki Eddy alitembea taratibu huku picha ya msichana katili anayejifanya mwema, Doreen ikizidi kumjia akilini mwake na kumfanya aisahau kabisa njaa aliokuwa nayo. Njia nzima alkuwa akizungumza peke yake kama mwehu mpaka alipofika bwenini.

"Ah Doreen! ni msichana mzuri sana! siamini kama amekuwa wangu..!" Aliwaza Eddy huku akiachia tabasamu kisha akabadili nguo na kujitupa kitandani. 

Alionekana kutoguswa kabisa na msiba wa mwalimu mkuu kwani tayari alikuwa amechanganyikiwa na Doreen. Hakumkumbuka tena Dorice ambaye kila Mara alimuahidi kutomsaliti kwa namna yoyote.

*******
Dorice alikuwa amekaa kitandani kwake huku machozi yakitiririka mashavuni mwake. Weupe wa ngozi ya USO wake ulibadilika na kuwa mwekundu kutokana na kulia kwa muda mrefu, hakuamini kama Eddy angemtenda kiasi kiasi kwani siku zote aliamini Eddy ndiye MTU pekee wa kumuamini, aliamini kama Eddy ndio furaha pekee ya moyo wake iweje Leo amtupe kama taka ya msafiri ndani  ya basi pale airushapo kupitia dirisha bila kujua itakapotua? Alimuona Eddy kama mnyama katili asiyekuwa na moyo wa utu.

Marafiki zake Dorice walizidi kumbembeleza atulie bila mafanikio yoyote.

"Kwa alichonifanyia Doreen, siwezi kumwacha kilahisi tu... lazima nimfanyie kitu..." Alijiapiza Dorice

" Ni lazima atajuta mpaka kifo chake... hatokaa anisahau kwa ntakachomfanyia.. lazima aelewe kuwa Mimi ni Dorice mtoto wa Kinyaturu sinyang'anywi tonge mdomoni kwa urahisi!" Alizidi kujiapiza Dorice akiwa amejifunika blanket mpaka usoni. Lakini baada ya muda mfupi Dorice aliinuka kitandani pale na kujifuta machozi kisha akapiga hatua za haraka kuelekea nje.

********
Mke wa Mwalimu John amuijia Juu Mumewe akitaka kujua suruali ile imetoka wapi. Lakini mwalimu John hakutaka kuweka wazi kile kilichomkumba shuleni.. alitaka iwe siri yake mpaka atakapofanikiwa kwenda Malawi kutafuta waganga wakumroga aliyemfanyia uchuro.

"John! umefumaniwa huko sio?" alifoka mke wa John
"usipaniki mke wangu tulia.. sijafumaniwa mim!" alijitetea mwalimu John bila mafanikio na wakati huo tayari mkewe alishaanza kumtandika makofi mumewe na alipoona haitoshi akanyanyua upawa na kumtandika nao Mwalimu John kichwani.

Ghafla John akanyong'onyea na kutulia kimya kitini bila kutikisika..
"John! John!" aliita mke wa mwlm John bila mafanikio John hakuweza kuitikia.
"Mime wangu... John wangu" alizidi kuita lakinu John alikuwa kimya, mkewe alichanganyikiwa sana.............

Itaendelea ......