RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TANO

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Tano
Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia sehemu ya Nne ( kama hukuisoma BOFYA HAPA  )
"hivi we demu unajisoma??" alisema Eddy kwa ukali. maneno hayo yalimshtua sana Dorice.
"Eddy! sijakuelewa!"
" unajisoma kweli? hivi kwanza unajua majamaa wanakucheka kwa sababu gani?" maneno ya Eddy yalimfanya Dorice .....
SEHEMU YA 5
...DORICE alimtazama Eddy kwa mshangao wa hali ya juu kwani tangu walipoanza mahusiano hakuwahi kumuona akiwa na chuki dhidi yake kwa kiasi kile. Dorice alikosa ujasiri wa kuzungumza chochote kwa wakati ule kwani alihisi viungo vyake vyote vinakosa nguvu. Akabaki ameduwaa kama zuzu mbele ya Eddy.
"we Dorice nimekuuliza unajua wanakucheka nini darasani?" aliuliza Eddy kwa ukali.
"Sijui" alijibu Dorice kwa huzuni
" Sasa kama hujui wanakucheka jinsi ulivyomchafu, hebu jiangalie hizo kamasi ulizojipaka kama mtoto asiyejua hata kutembea, pili hiyo yako chafu, na tatu...." kabla Eddy hajamaliza Dorice alishtuka sana kusikia vile kwani alipofika darasani asubuhi alikuwa msafi kama ilivyokuwa kawaida yake.
"Eddy umesemaje?!" aliuliza Dorice kwa mshangao. Na wakati huo Doreen alikuwa alikuwa amejificha nyuma ya darasa karibu na waliposimama akina Dorice, na aliweza kusikia kila kitu kinachozungumzwa. Alisikiliza kwa umakini sana huku akiyafurahia majibu ya Eddy Kwa Dorice.
" Hujanisikia? tena ukome kunifuatilia, usahau kama nilishakuwa mpenzi wako , unifute akilini mwako, sikupendi?" alisema Eddy akiwa amenuna kama aliyekula ndimu.
"unasemaje Eddy! hebu rudia nisikie"
"Sikutaki , sikupendi na sikuhitaji!" alisema Eddy huku akiondoka
"Eddy! Eddy! nimekukosea nini mpenzi wangu?"
"Achana na Mimi Dorice! huna hadhi ya kuwa na mimi , demu mwenyewe huna hata mvuto!" alisema Eddy na kusonya. Kisha akaenda zake darasani.
Alimwacha Dorice kwenye bahari ya simanzi na machozi yasiyoweza kuzuilika. Alilia kwa uchungu kama MTU aliyefiwa na MTU muhimu, lakini kilio hicho cha Dorice kilikuwa shangwe na furaha kwa Doreen. Alijiona kama mshindi kwa kufanikiwa kulivuruga penzi la Eddy na Dorice bila hata huruma kwani wawili hao walipendana sana na walikuwa na malengo makubwa katika maisha ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa pindi watakapotimiza malengo yao.
Doreen alicheka kwa dharau kisha akaondoka zake na kwenda darasani, ambapo alimfuata Eddy pale alipokuwa amekaa.
Eddy alimkaribisha Doreen kwa tabasamu mwanana na macho ya matamanio.
"Mambo Eddy handsome" alisema Doreen kwa sauti ya utulivu iliyomkuna vyema Eddy hadi akakosa ujasiri wa kuongea.
"Eddy mbona huitikii salam yangu?"
"Niko poa... vipi wewe mtoto mzuri"
"mh! nani mzuri Eddy?" Doreen alijifanya kuona aibu. Na kwakuwa darasa lilikuwa na kelele nyingi walipata mwanya wa kuzungumza zaidi.
"mzuri wewe hapo mtoto wa kitanga!"
"Acha hizo Eddy! mzuri no Dorice!"
"Eh! usinitajie huo uchafu"
"mh! uchafu tena? "
"ndio... Doreen bora umekuja hapa kukaa.. nina kitu muhimu sana nataka nikwambie"
"mh! kitu gani Eddy?" aliuliza Doreen huku akirembua jicho lake kubwa zuri kwa madaha.
***
Karatasi lile lenye ujumbe mzito lilitua mikononi mwa mtaaluma wa shule, kwa haraka macho yake yalitua kwenye maandishi yaliyoandikwa kwenye karatasi ile lakini maandishi yalikuwa tofauti na yale aliyoyasoma makamu mkuu wa shule, yalisomeka hivi "TOENI HUO MZOGA LA SIVYO MTAISHA"
Mwalimu yule wa taaluma aliogopa sana akashindwa kuongea akampasia karatasi mwalimu wa nidhamu lakini alipochukua tu ujumbe ulibadilika ukasomeka hivi "WEWE UTAMFUATA MAKAMU WA SHULE MAANA ULINITESA"
"ati nin? nilikutesa wapi Mimi? hata sio Mimi ujumbe haunihusu!" mwalimu wa nidhamu aliongea kwa kuchanganyikiwa na kwa hofu kubwa. Akampasia karatasi mwalimu mwingine lakini pindi anapompa mwalimu yule karatasi ujumbe ulibadilika tena "MNANISUMBUA! UKIMPA MWINGINE UJUMBE HUU UNAKUFA MUDA HUU.. NA UKINIWEKA CHINI UTAONA CHA MTEMA KUNI"
Mwalimu yule aliyefahamika kwa jina la mwalimu Jason alivuta pumzi ndefu sana huku mapigo ya moyo yakibadili mwendokasi na kwenda haraka sana. Akabaki ameshikilia karatasi lile mkononi mwake bila kuelewa cha kufanya .
WAlimu waliokuwa wanasubiri kusoma karatasi lile walimfokea mwalimu Jason kwa kuendelea kulishikilia karatasi lile kabla ya wao kulisoma.
"we vipi tupe na sisi tusome!"
"shukuru hamjasoma"
"Nini? usituzingue tupe hilo karatasi tusome bhana"
walimu walizidi kung'ang'ania karatasi lile lakini mwalimu Jason hakuwa tayari kuwapa ili kulinda uhai wake. Mwalimu Jasoni akaangalia upenyo ili aweze kutoka ofisini mle kisha akatoka mbio akiwa ameshikilia karatasi lake.
Mwalimu wa taaluma akaangalia pale chini ulipokuwepo mzoga wa Mbeshi akaona jinsi funza wallivyokuwa wakitapakaa kwa kasi.
"Jamani tumtoeni huyu tutakufa wote"alisema mtaaluma.
wakati huo makamu mkuu wa shule alikuwa akitokwa na haja ndogo kutokana na hofu ya kifo kama alivyoambiwa kwenye ujumbe.
***
Mwalimu John alionekana mwenye sana pindi aliporudi nyumbani kutokana na kitendo cha kudhalilika shuleni. Mkewe aliingia sebuleni na kumsogelea mwalimu John
"mume wangu vipi?"
"kwani vipi mke wangu?"
"nakuona hauna raha kulikoni?"
"nipo sawa... Ila... nina safari..!"
"kha! safari ya wapi tena mume wangu?"
"Naenda Malawi... Leo!"
"Malawi? kufanya nini mume wangu?"
"usijali kuna kazi muhimu naenda kufanya.."
"mbona ghafla sana? halafu mbona umevaa suruali ambayo si yako? au umefumaniwa?"
Aliuliza mke wa mwalimu john huku akimkagua mume wake kwa kupitisha macho kuanzia juu had I chin... ...
Itaendelea ......