RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 22

RIWAYA:A WIZARD STUDENT (MWANAFUNZI MCHAWI)
MTUNZI: ENEA FAIDY

SEHEMU YA 22

..MR ALLOYCE alishtuka sana baada ya kusikia kishindo kalikali nyuma yake. Aliachia chupa ya konyagi kisha
akageuka haraka kutazama nini kinaendelea nyuma yake. Hakuamini kumuona mwanaye akiwa amejibwaga chini kama gunia la viazi. Alikuwa anathema kupita maelezo.
"Eddy!" Mr Aloyce aliita kwa mshangao mkubwa. Lakini Eddy hakuitikia zaidi ya kuendelea  kuhema kwa nguvu.
Mr Alloyce alitupa chini vidonge alivyokuwa amevishika, akamwinamia Mwanaye na kumgusa kifuani ili kusikiliza mapigo ya moyo. Aligundua kuwa mwanaye ni mzima alimsgukuru Mungu. Killed home hang a za Mr Alloyce ni kwamba pindi anarudi sebuleni pale, hakukuta mtu yeyote na wala hakusikia mtu akifungua mlango. 
"Ba...ba..!" Aliita Eddy kwa shida sana.
"Sema mwanangu...Mimi hapa" aliitikia Mr Aloyce.
"Usife. .!"
"Sifi nani kasema Mimi nakufa? Vipi lakini uko sawa?" Aliuliza mr Alloyce akiwa na hofu sana, alihofia kumpoteza mwanaye kipenzi. Eddy aliitikia kwa kichwa tu akimhakikishia baba yake kuwa yuko sawa.
Mr Alloyce aliendelea kumkagua Mwanaye kila sehemu akidhani labda ana majeraha kwani damu alizozikuta chumbani kwa Eddy zilimtisha Sana. Lakini alipomtazama mwanaye akagundua hana jeraha lolote mwilini mwake, hivyo maswali mengi yalijitokeza akilini mwake. Alijihoji maswali mengi lakini hakuwa na majibu yake.
"Baba... Mama anateseka sana!" Eddy aliongea sauti ndogo ya kujivuta sana akiwa bado amelala pale sakafuni.
"Anateseka wapi?" Mr Alloyce alishtuka sana.
"Alikuja hapa..  Anateseka sana na yote kwa sababu yangu...!" Alisema Eddy kwa huzuni sana huku machozi yakimlengalenga machoni.
"Eddy! Upo sawa kweli?" Mr Alloyce alihisi Eddy hayupo sawa hivyo anaropoka tu anachojisikia.
"Nimefanya makosa sana.. Namtesa mama yangu..."
"Eddy usiseme hivyo.. Unamtesa na nini?"
"Alivyotaka kunipeleka kwa mganga wameamua kumuadhibu...!"
"Kina nani?"
"Wachawi...!"
"Oh My God.." 
Maneno Yale yalizidi kumchanganya Mr Alloyce, alishundwa afanyaje kwani ilikuwa ni Mara yake ya kwanza maishani mwake kukumbana na mauzauza ya namna ile. Mara nyingi alizoea kutazama kwenye luninga tu lakini hakujua kama inaweza kumtokea kweli. Maisha yake yalikuwa machungu ndani ya muda mfupi tu kwanu matatizo aliyokuwa NAyo yalikuwa mazito tena yanaumiza kama gunia la misumari.
"Baba.. Nakupenda..!"
"Nakupenda pia mwanangu!"
 Mr Aloyce alijikuta anashusha mchozi tu kila anapomtazama mwanaye kwanu siku zote aliamini mwanaye atakuwa mtu mkubwa sana kutokana na uwezo wake darasani. Alikuwa na akili nyingi lakini Leo amekuwa mtu wa kuteseka tu. Aliwachukia wanadamu wenzake kwa ukatili wanaoufanya juu ya familia yake.
"Baba.."
"Naam mwanangu.."
"Chukua hii." Eddy alimkabidhi baba yake kipande cha karatasi.
Mr Aloyce alishtuka kidogo kisha akapokea karatasi like na kulikunjua ili alisome. 

Ujumbe uliokuwepo pale ulimshtua  sana Mr Alloyce. Aliurudia tena
"CHAGUA MOJA.
EDDY APONE TATIZO LAKE, MAMA YAKE APOTEE DAIMA. AU MAMA EDDY ARUDI, EDDY ABAKI NA TATIZO LAKE"
MR Aloyce alibaki mdomo wazi kwa mshangao, kwani ule ulikuwa mtihani mgumu kwake.
"Karatasi limetoka wapi?"

****

Mama muuza mgahawa alikuwa kama mwehu baada ya pesa zake kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Aliambatana na mfanyakazi wake ili wamfate Doreen. Waliifuata njia aliyoelekea Doreen na kumtazama huku na kule lakini licha ya kumfuatilia kwa muda mrefu hawakufanikiwa kumuona. Walifika mpaka kituo cha mabasi kumtafuta lakini pia hawakumuona.
"Luna msichana alipita hapa, mweupe amevaa sweta jeusi na sketi ya kahawia?" Aliuliza Fetty mfanyakazi wa yule mama muuza mgahawa.
"Ni mzuri sana?"
"Ndio!"
"Alipanda basi la Mbeya na limeondoka!"
Aliwajibu kijana mmoja ambaye alionekana ni kondakta wa basi.

Yule mama aliangua kilio kikali palepale kwenye kituo cha mabasi bila kujali wingi wa watu. Alilia kwa sauti Kali akiwa ameweka mikono kichwani. Watu walimshangaa mama yule wakaanza kumkusanyikia.
"Hela zaangu.. Hela zaaangu... Nitalipa nini  Mimi...!"
"Mama twende basi..!"
"Nataka hela zangu... Nitafanyaje hela za watu.. Hela za mkopo" 
Alilia mama yule kwa uchungu na hasira nyingi. Watu waliendelea kumshangaa pale, lakini tayari alikuwa amelizwa na binti Doreen.

Huku mama yule akiwa analilia pesa zake, Doreen alikuwa na furaha sana kwa kupata pesa zile kwani zilimsaidia katka nauli ya kutoka Iringa kwenda Mbeya.

Doreen hakuwa na ndugu yeyote jijini Mbeya ila aliamua kwenda Huko kwaajili ya kukamilisha kazi zake hasa hasa ikiwa kupata titi la msichana mrembo.

Akiwa ndani ya basi, Doreen hakuweza kuzungumza na MTU yeyote. Alitulia kimya akiwa amejiinamia. Alionekana mwenye mawazo mengi sana tena mwenye huzuni kupita kiasi. Jirani yake Doreen ambaye ni mwanamama wa makamo kiasi kama miaka 40 au 45 alimuona Doreen akiwa katika hali ile. Alimwonea huruma na kuamua kumuita.
"We binti hujambo!" Alisema mama yule lakini Doreen alibaki kimya kama vile hakusikia anavyoitwa.
"We mdada!" Aliita na kumgusa began Doreen. Doreen aliinua kichwa na kumtazama mwanamke yule.
"Shkamoo mama!" Doreen alimsalimia  kwa heshima na adabu mwanamke yule.
"Marhaba.. Mie naitwa Bi Carolina.. Unaitwa nani?"
"Naitwa Doreen!"
"Asante.. Mbona una mawazo sana? Tangu umeingia kwenye gari huna raha hata kidogo.. Una tatizo gani?" Aliuliza mwanamke yule kwa upole sana.
"Nina matatizo makubwa sana mama?" Alisema Doreen kwa unyonge wa hali ya juu.
"Tatizo gani?"
"Ni hadithi ndefu sana mama angu!" Alisema Dorice safari hii machozi yalimlengalenga machoni. Maneno Yale yalivuta usikivu wa Bi Carolina. Alitamani amsikilize zaidi.
"Mama! Acha tu..  Dunia ina mateso sana..! Sins hamu!" Doreen aliachia mchozi uliokuwa ukimlengalenga machoni. Bi Carolina alimtazama kwa huruma Doreen na kumtaka aendelee kumsimulia.
"Mama! Iringa nilikuwa naishi na mjomba wangu, tumbo moja na mama yangu! Na alinichukua baada ya wazazi wangu kufariki, aliahidi atanisomesha lakini hakufanya hivyo. Alikuwa akininyanyasa, hanipi chakula, ananifanyisha kazi ngum wakati anajua kabisa naumwa moyo, jana kanifukuza usiku wa manane akidai namchafulia hali ya hewa nyumbani kwake, sina hadhi. Nimeteseka sana, sins hata kwa kwenda!" Alisema Doreen kwa uchungu huku akilia. Simulizi yake ilimuumiza sana Bi Carolina akatamani kumsaidia Doreen.
"Pole sana Doreen.. Kwahiyo Mbeya unaenda kwa nani?"
"Sina ndugu huko.. Naenda tu hata kutafuta vibarua..!" Aliendelea Julia Doreen akachukua leso yake na kujifuta machozi.
"Dash pole sana.. Kwangu naishi na mume wangu na binti yangu.. Naomba nikusaidie ukaishi kwangu.." Alisema yule mama kwa huruma sana.
Doreen alifurahi sana kimoyomoyo has a alivoambiwa kuna binti anaishi pale...

ITAENDELEA..
KAMA WEWE UNGEKUWA ALOYCE UNGEFANYAJE??

UNAMSHAURI NINI BI CAROLINA?

LIKE, COMMENT , SHARE

2 Comments

  1. Da hip ni mtihan mzito hapo ni kumuomba mungo tuu daa inatiisha sana

    ReplyDelete
  2. Daa Hatar sana stori Nzuri ila inatisha

    ReplyDelete