RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Riwaya:Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard) - Sehemu ya Kumi na moja
MTUNZI: ENEA FAIDY
...Jeneza la mwalimu John lilikuwa tayari limefunuka, Mwalimu John aliinuka ndani ya Jeneza na kusimama wima cha kwanza alichofanya ilikuwa ni kunyanyua kinywa chake na kumuita mkewe mpenzi kwani ndiye aliyekuwa akimfikiria kila sekunde. " Mke wanguuuuu... Niko hai..usilie" Mwalimu John alisema kwa sauti kuu, huku furaha ikiwa imefurika moyoni mwake kwani hakuamini kama kweli ameurudia uhai.
Akiwa katika furaha hiyo isiyo na kikomo mwalimu John akatahamaki sana baada ya kuona umati wote uliokuwa ukiomboleza kwaajili yake ukikimbia. Watu walikimbia kwa fujo huku hofu ikiwa imewatamalaki. Cha ajabu hata mke wa Mwalimu John pia alikimbia kama swala anayekabiliana na mnyama mkali.
Hakuna aliyesalia kwenye eneo lile, vumbi lilitimka na kuwaaga waombolezaji wote ambao mpaka wakati ule hakuna aliyejua kilichotokea. "Maajabu haya! Maiti kafufuka? Kweli dunia IPO ukingoni" alisikika mwanamume mmoja ambaye alikuwa amejikwaa mguu baada ya kukimbia kwa muda mrefu.Alihema kwa nguvu huku akizitafuta nguvu zingine za kukimbilia. Ghafla akahisi kuna Mtu kasimama nyuma yake
" Vipi kuna mini kwani?" Ilisikika sauti ile ambayo ilipenya vyema masikioni mwa mwanaume yule. Akageuka kutazama anayeuliza, Mwanaume yule alitetemeka sana baada ya kukutana USO kwa uso na Mwalimu John. Akainuka haraka na kuziendeleza mbio zake.
Mwalimu John alikuwa haelewi ni kwanini watu wote wanakimbia, na yeye akaingiwa na hofu akaanza kukimbia akijua labda kuna jambo la hatari linakuja. Alizipiga mbio kuelekea nyumbani kwake ili akajihifadhi haraka iwezekanavyo.
Mwalimu John alipofika mtaani kwao, kila MTU alikimbilia ndani na kujifungia. Ndipo alipozidisha juhudi na kuongeza mwendokasi akidhani hatari inamkaribia. Mwalimu John alifika nyumbani kwake, alipofika getini ghafla geti likafungwa. Akastaajabu sana kwani hakufikiria kuwa mkewe badala ya kumpokea kwa shamrashamra alimfungia mlango.
" Nifungulie mke wangu!" Alisema Mwalimu John huku akipigapiga mlango, na kwakuwa mlango haukufungwa vyema ukajifungua. Mwalimu John aliingia ndani huku akihema sana.
"Mamaaaaa!"
Zilisikika kelele ndani ya nyumba ya Mwalimu John, ndugu wote walipiga kelele.
"mke wangu! Hunitaki!?" Mwalimu John aliuliza kwa sauti ya kutia huruma, huku akimsogelea mkewe.
"Ushindweee!" Mkewe alifoka.
"Mke wangu nishindwe Mimi? Leo unaniambia nishindwe kwani Mimi pepo?" Mwalimu John alizidi kutia huruma.
Aliinamisha kichwa chini, kwa bahati macho yakatua mwilini mwake. Mwalimu John alishtuka kupita kiasi, akajiogopa na akatamani kujikimbia.
"Nooooooooo!"
*****
Eddy alikuwa yupo kwenye wakati mgumu sana , alishindwa kujua lipi ni sahihi kichwani mwake kati ya kifo au kuishi kwa aibu.
Alikuwa bado ameshikilia vidonge huku machozi yakimchuruzika kama bombs machoni mwake. Alilia kwa uchungu huku akimlaani sana Doreen, alimuona kama mnyama aliyekuja kuupoteza uhai wake. Alimchukia kuliko kitu kingine chochote lakini tayari alikuwa amechelewa.
"I wapi thamani yangu? Edd mie ninaetegemewa na wazazi wangu! Siwezi kuishi tena.. Bora nife tu kuliko kuishi kwa fedheha hapa duniani!" Mawazo hayo yalipita taratibu kichwani mwa Eddy. Hatimaye kichwa chake kikafanya maamuzi akaamua kujiua.
Kabla hajatupia lundo la vidonge vile kinywani, mlango ulifunguka. Hatua za miguu kulekea aliko Eddy zilimshtua. Jakson akiambatana na Zawadi walifika pale alipo Eddy, walishtuka sana kukuta vidonge vingi vikiwa mkononi mwa Eddy.
"Eddy vipi unataka kujiua" Jackson alisema kwa mshtuko huku akimnyang'anya kinguvu vidonge vile.
"Acha nife tu!" Alisema Eddy kwa unyonge.
"Huwezi kufa, na huwezi amini Eddy nimempigia simu mama yako nimemwambia una matatizo aje kukuchukua!"
"What! Sitaki Mimi! Sipendi kiherehere chako Jack! Umemwambia nini?"
Eddy alifoka kwa hasira.
"Hebu tulia bro! Mimi sijamwambia bays lolote, nimemwambia una matatizo ambayo hutaki walimu wajue, na sio muda anakuja!"
"Umenikera sana ujue, sitaki kwenda home! Bora ningekunywa dawa zangu mapema kabla haujafanya huo ujinga wako.. Sio siri kaka umeniboa kinazi!"
Alizidi kufoka Eddy.
"Eddy haupo sawa.. Jack usimsikilize huyu sio kosa lake! " alisema Zawadi.
"Nani hayupo sawa unamaana nina kichaa sio? Nyie wote mabwege tu.. Siwaelewi wala nini.." Eddy alikuwa kama mwenda wazimu, Jack na Zawadi walitulia kimya tu.
"Nawaharibia sasa hivi mjue! Niondokeeni hapa.. Poteeni maboya nyie..!"
Jackson na Zawadi walitulia kimya tu, ghafla meseji iliingia kwenye simu ya Jackson. Ingawa simu zilikuwa haziruhusiwi shuleni pale ila alikuwa na simu ya kimagendo.
"Nimefika hapa shule mwanangu!"
Ilikuwa ni meseji kutoka kwa mama yake Eddy kwani alikuwa amewasiliana na patron ambaye alikuwa anafahamiana nae vizuri hivyo waliyamaliza.
Hazikupita hata dakika kumi Eddy alikuja kuchukuliwa bwenini. Alikuwa na hali mbaya sana kwani alikuwa kama mwenda wazimu.
Mama take alipoletewa kijana wake hakuamini.
"Eddy mwanangu wakufanya nini? Wamekupa kichaa?" Alisema mwanamama yule mrembo.
"Siendi kokote mie, siendi na mtu!" Eddy alikataa kuondoka . Ikabidi wambebe kinguvu na kumsweka kwenye gari ya mama yake.
"Mungu wangu mtoto mwenyewe mmoja huyu kama roho.. Mungu wangu wee!"
Alilia Mama Eddy.
****
Doreen alisikia taarifa za kuondoka kwa Eddy, roho ilimuuma ila hakuwa na jinsi alijifanya kuhuzunika na wenzake kumbe yeye ndiye aliyefanya kila kitu.
Alitamani kuondoka mapema kabla siri zake hazijafichuka lakini alikuwa amebakiwa na kazi moja kubwa sana. Alitakiwa achukue titi moja la msichana mrembo sana shuleni pale ili akamilishe kazi yake.
Alijiuliza sana achukue titi la nani bado ulikuwa mtihani kwake. Akajilaumu kwanini hakuchukua titi la Dorice kwani ingekuwa kazi rahisi kwake.
" Nilizembea sana! Sasa nifanyaje?" Alijiuliza Doreen.
Baada ya kuumiza kichwa kwa muda mrefu hatimaye alipata jibu. Picha ya msichana mzuri aitwaye Nadia Joseph ilimjia kichwani. Alikuwa in msichana mzuri sana kwa sura, umbo mpaka tabia.
"Wow! Atanifaa sana! Na vile vititi anavyovibust vile.. !" Doreen alitabasamu akijua tayari kazi imeisha. Ushindi ni wake. Alifurahia sana kumfanyia mwenzie ukatili.
Kilichobaki ilikuwa ni kusuka mipango ili mambo yake yaende sawa.Aliinuka kitini na kumfuata Nadia Joseph darasani, alimkuta binti yule mwenye sura ya upole na werevu akiwa ametulia kimya kwenye dawati lake akiendelea kujisomea.
"Mambo mrembo!"
"Poa.. Habari yako?"
"Salama.. Nimekuja kupiga stori na were, vipi upon tayari?"
"Karibu.." Alisema Nadia Joseph huku akimkazia macho Doreen.
"OK!"
Wakati Doreen akikakaa, Nadia alihisi kitu.. Tens kitu kibaya sana! Machale yakamcheza kwa kasi sana akajua hakuna usalama wowote kwa Doreen. Haraka sana akaamua kuchukua hatua.......
HAPO SASA DOREEN KAKUTANA NA MOTO WA MAKUTI UNAFIKIRI NINI KITAENDELEA?... USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU INAYOFUATA.