RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 21

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya Ishirini na Moja
MTUNZI: ENEA FAIDY
... MR ALOYCE alichanganyikiwa sana baada ya kukuta damu ikiwa imetapakaa sakafuni chumbani kwa mwanaye. Alipigwa na butwaa huku hofu ya kuondokewa na mwanae ikiwa
imemvaa ghafla.
"Eeeddy!" Alijikuta anaita kwa sauti Kali ili kama Eddy yupo mbali asikie na aitikie wito ule ambao ungemwondolea wasiwasi Mr Alloyce. Lakini wito ule haukuitikiwa na mtu yoyote zaidi ya ukimya uliokuwa umetawala ndani ya jumba lile la kifahari.
Mr Alloyce alijaribu kuita tena na tena lakini bado hakuitikiwa. Simanzi ikamjaa tele, akajua tayari amepata pigo lingine zito kabla hata kidonda cha mwanzo hakijapona kwani ndio kwanza kilikuwa kibichi.
"We Mungu wangu nimekukosea nini Mimi mbona unaniadhibu hivi? Nihurumie uikomboe familia yangu" alilia mr Alloyce akiwa amejibwaga sakafuni kwenye korido ya kuelekea sebuleni. Machozu yalimchuruzika kama mvua huku yakiteremka kama vijito kuelekea kwenye marumaru za rangi ya maziwa zilizochanganyika na weupe.
"We Mungu nitaishi vipi Mimi na upweke huu? Sina mke, sina mtoto?" Alilalamika kwa majonzi mr Alloyce. Aliwaza mengi sana yaliyozidisha simanzi yake moyoni, moyo wake ukajawa na maumivu makali sana kama mtu aliyechomwa na mkuki wa moto katikati ya moyo wake.
"Bora na Mimi nife kuliko kubaki kwenye hali kama hii...!" Aliwaza Mr Alloyce kisha akainuka pale sakafuni na kuelekea chumbani kwake. Aliingia chumbani na kuwasha taa, kisha akaisogelea droo ya dressing table akaifungua na kuanza kupekuapekua vitu.
Alipekua kwa muda kisha akapata karasi ya ranging ya kaki akafunua kwa umakini kisha akazikuta dawa alizozihitaji. Kulikuwa na vidonge Vingi sana ndani ya pakiti ile kaki, akavibeba na kuirudisha droo kama ilivyokuwa akatoka kuelekea sebuleni.
Alifika sebuleni na kuliendea jokofu ili achukue pombe Kali anywe pamoja na vile vidonge ili aondokane na ulimwengu huu wa mateso ambao alihisi umemtenga baada ya kumtenganisha na wapendwa wake. Akiwa anafungua jokofu na kichukua chupa moja ya konyagi ghafla alishtuka sana.
*****
Dorice aliyastaajabu mazingira aliyopelekwa kwani palikuwa na viumbe wengi wa ajabu ambao yeye hakuwahi kuwaona hats siku moja.
Ulikuwa kama ukumbi mkubwa sana uliotawaliwa na viumbe wale wa ajabu, alipopiga jicho mbele ya ukumbi ule aliona viti viwili vyenye rangi ya shaba vikiwa vimetengwa peke yake. Alimtazama Mansoor kwa sura ya maswali lakini Mansoor hakuzungumza neno lolote zaidi ya kumshika mkono Dorice na kuongozana nae mpaka kwenye vile viti. Walipovifikia tu, ghafla akatokea kiumbe mmoja wa kutisha sana kwani alikuwa na macho kama ya bundi, meno marefu yaliyochongoka na kucha ndefu za miguuni na mikononi. Mwili wake ulitawaliwa na manyoya na kila alipozungumza kinywa chake kilitema moshi mweusi. Doreen aliogopa sana, akajikuta anamsogelea Mansoor kwa hofu.
"Usiogope Mpenzi... Huyu ni mfungishaji ndoa!" Mansoor alimtoa hofu Dorice. Dorice alibaki kimya huku moyo wake ukibaki na woga wa hali ya juu.
"Leo ndio ile siku tuliyoisubiri kwa hamu sana, hatimaye kijana wetu mtoto wa mtukufu malkia amepata mwenza wake wa maisha!" Alisema kiumbe yule wa kutisha. Radi Kali zilipigwa ishara ya kufurahia kile kinachozungumzwa.
"Bi Aisha utakuwa mke halali wa Mansoor... Kwa kuivaa Pete hii ambayo hutakiwi kuivua maisha yako yote." Alisema kiumbe yule huku akimkabidhi Mansoor Pete nzuri sana ya dhahabu, iling'aa kupita kawaida.
"Nakupenda sana, nakuoa leo, naahidi kukulinda Siku zote kama mke wangu. Tafadhali sana usije ukaivua Pete hii hats Mara moja!" Alisema Mansoor na kumvisha Pete Dorice. Dorice alikuwa anaogopa sana, machozi yalimlengalenga machoni kwani hakuamini kama kweli anaolewa na jini.Ndoa ilifungwa na Dorice alipewa onto la kutoivua Pete yake ya ndoa hata Mara moja.
*****
Doreen alimkabidhi pesa ile muuz mgahawa kisha akaendelea kula chipsi zake kwa haraka sana utadhani anakimbizwa na polisi, hata kabla ya kumaliza akaziacha mezani pale na kumfuata yule mama muuzaji kisha akamdai chenji.
Mwanamama yule alitoa shilingi mia tatu kwenye pochi ndogo aliyokuwa akihifadhi pesa kisha akamkabidhi Doreen. Lakini cha ajabu baada ya kumkabidhi tu Doreen pesa zile, kitita cha pesa zote alizouza siku ile zikaenda kwa Doreen bila yeye mwenyewe kujua. Zilikuwa kama elfu sitini na tatu halafu yeye akabakiwa na shilingi mia tatu.
Doreen alipozichukua pesa zile akapiga hatua kubwakubwa kuelekea kituo cha mabadi kwani tayari alikuwa amepata nauli na pesa ya kutumia njiani kuelekea mkoani Mbeya.
Yule mama aliendelea na shughuli zake kama kawaida, alimhudumia mteja mmoja kisha mteja yule alimpa shilingi elfu kumi na akahitaji chenji. Bila wasiwasi mwanamke yule aliiendea pochi yake na kutaka kuchukua hela lakini alipoishika tu pochi ile akahisi kitu, maana pochi ilikuwa nyepesi kuliko kawaida. Alishtuka kidogo kisha akaifungua. Hakutaka kuamini macho yake kwa alichokiona.
"Hela zangu!!!!!!" Aliongea kwa mshtuko mkali kisha wote wakamtazama mama yule .
"Hela zaaangu mieee!" Alianza kushusha kilio huku akizitafuta huku na kule lakini hakuziona.
"Fety wapi hela zangu?" Mama yule alimuuliza mfanya kazi wake.
"Hela? Si uliziweka humo?"
"Ndio mbona sizioni sasa? Sema tu kama umechukua! Hakuna mwingine ni we we Fety..!' Mama yule alilia huku akimkunja mfanyakazi wake akihisi ndiye aliyemwibia.
"Mama tangu lini nimekuibia?"
"Nani angechukua!? Nani nakuuliza?" Mama yule aliongea kwa hasira sana.
"Sio Mimi mama unanionea Bure..!"
"Na utanilipa shenzi wewe..!" Alizidi kumkunja.
"Labda umemzidishia yule mteja aliyeondoka?"
"Tutamfata kama si yeye utanikoma..!" Aliongea kwa hasira sana mama yule kwani mtaji wote alikuwa amechukua pesa za mkopo. Hivyo alichanganyikiwa sana.
Waliamua kumfuatilia Doreen kule alikoenda. ...
Itaendelea.....
Usikose kufuatilia

1 Response to "RIWAYA YA MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA 21"